Mwandishi afariki dunia

Mtangazji Mkongwe wa Zanzibar Bw.Joseph Caitan Asama (79) amefariki dunia jana mchana nyumbani kwake Mbweni nje kidogo ya Mji wa Zanzibar.Misa ya Marehemu Asama itafanyika kesho mchana katika kanisa la Anglikana Mbweni na kutarajiwa kuzikwa katika makaburi ya Mwanakwerekwe Zanzibar saa tisa kamili alaasiri.

MTANGAZAJI Mkongwe wa Zanzibar Joseph Caitan Asama (79) amefariki dunia jana mchana nyumbani kwake Mbweni nje kidogo ya Mji wa Zanzibar.

Marehemu Asama alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa moyo kwa muda mrefu na alizidiwa jana mchana wakati akiwa katika matayarisho ya kukimbizwa Hospitali Kuu ya Mnazi Mmoja kwa matibabu na hatimae kufariki dunia.

Misa ya Marehemu Asama itafanyika kesho mchana katika kanisa la Angilkana Mbweni na kutarajiwa kuzikwa katika makaburi ya Mwanakwerekwe wilaya ya Magharibi Unguja saa 9:00 za alaasiri.

Viongozi mbali mbali na maafisa wa ngazi ya juu wa serikali pamoja na wananchi wanatarajiwa kuhudhuria katika mazishi ya mtangazaji huyo Mkongwe wa Sauti ya Tanzania Zanzibar (STZ) ambaye ameitumikia kwa muda mrefu katika uhai wake.

Marehemu Asama alianza kazi katika miaka ya mwishoni mwa hamsini (50) katika Idara ya Habari na Utangazaji akiwa katika sehemu ya utangazaji ya Sauti ya Unguja kabla ya kuwa Sauti ya Tanzania Zanzibar (STZ).

Ukiacha uzoefu katika utangazaji, Marehemu Joseph Asama alikuwa Mkuu wa vipindi wa Sauti ya Tanzania Zanzibar (STZ), Mwandishi wa habari wa Rais wa Zanzibar na Makamo wa Kwanza wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mzee Aboud Jumbe Mwinyi.

Nafasi nyengine ambazo alishika wakati wa uhai wake ni Mkurugenzi wa Idara ya Habari na Utangazaji pamoja na Afisa Uhusiano wa Kamisheni ya Utalii Zanzibar ambayo amemalizikia nayo kuitumia baada ya kustaafu kazi miaka ya hivi karibuni.

Marehemu Joseph Asama ametangulia nasi tupo nyuma yake na ameacha kizuka mmoja na watoto wawili, Mwenyeenzi Mungu ailaze mahali pema roho ya Marehemu Joseph Caitan Asama.

4 responses to “Mwandishi afariki dunia

 1. Mzee Asama alikuwa ni mtu wa karibu sana na jamaa na alikuwa sio mwenye kunughudhi wengine.

  Nimepata kufanya kazi alipokuwa utalii ikiwa mie nipo na Environment Impact Assessments (EIA). Siku mmoja aliniuliza ni Mazingira au Mazingara nikamwambia hivyo ni vitu 2 tafauti. Akisema Kiswahili kwa ufasaha na alikuwa na fluency ya Kiengereza ikiwa ni kumbukumbu za Government School chini ya walimu kama Davies, Hens na wengineo.

  Mola amlaze anapostahiki.

  Ben Rijal

 2. Huyu ni muandishi wa zamani sana. Ingelikuwa jambo la busara, kama inawezekana tukaiona picha yake.

 3. poleni kwa msiba mzito wazanzibari wote, lakini naomba niulize hivi haya majengo ya unguja mbona hayakarabatiwi!? Hayapakwi rangi! Tatizo ni nini!? Dada salma ukinijibu hata ktk inbox ya fb nitashukuru,

 4. Mimi natoka kwenye mada kidogo, linalonikera na kunisumbua ni Hili Kanisa la Mkunazini au Minara Miwioli?

  Tafadhalini nijibuni kama munajuwa ni kanisa gani? Lakini haswa nakusudia kusema kwamba hili kanisa ni moja ya Historical building ambalo hutia pesa nyingi za kigeni. Kwani Sio wageni wote huja kulala na kuogelea katika White Sands Beach . bali kuna wengi huja kutafuta historia ya Zanzibar.

  Na Umuhimu wa kanisa hili nikufanyiwa ukarabati wa ndani na nje na kupakwa rangi. Hii sio dhambi kufanya hivyo, kwani nikutunza utamaduni wetu na historia yetu. Sio hivo tu najuwa kwamba Makanisa ya Tanganyika/Tanzania yanapatiwa milklions ya pesa kila mwaka ambayo iko kwenye Budget ya Serikali ya Kitanganyiyika/ Tanzania.

  Hii nikwasababu yakuedeleza ukarabati wa majengo hayo wakati misikiti hawana budget yoyote ile. Sasa pesa hizo huwa zinatengezewa makanisa ya Ki-Bara tu na sio hayo ya Zanzibar? Kwanini? Hii sio moja ya kero kubwa za Muungano?

  Ndugu Wazanzibari tukumbuke Mji mkongwe ni moja wa Historia yetu kubwa hapa Zanzibar. Na umekuwa katika hifadhi za Dunia, ni haki yetu ku-utunza mji huu na majengo yake kwa hali na mali. Na moja ni hili la kupaka rangi majengo yote yna taasisi za Serikali zilipo Mji Mkongwe.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s