Ajira kwa waafrika zanukia

Nchi za Tanzania, Kenya na Uganda zinatarajiwa kupata ajira mpya 23,000 baada ya miaka mitano.Ajira hizo zitatarajiwa kuwanuisha jumla ya vijana millioni 1.2 ili kukabiliana na hali ya maisha na kuondokana na umasikini.

IMEELEZWA kwamba nchi za Tanzania, Kenya na Uganda zinatarajiwa kupata ajira mpya 23,000 baada ya miaka mitano.Ajira hizo zitatarajiwa kuwanuisha jumla ya vijana millioni 1.2 ili kukabiliana na hali ya maisha na kuondokana na umasikini.

Hayo yameelezwa na Mtaalam wa mpango wa kukuza ujasiliamali, Julius Mutio, kutoka nchini Kenya wakati akizungumza katika semina ya siku moja iliyotayarishwa na taasisi uanzishaji na ukuzaji wa shughuli za ujasiliamali kwa vijana (YEF) katika Hoteli ya Mazsons, Shangani Zanzibar.

Mutio alisema ajira hizo zinatarajiwa katika kipindi cha miaka mitano ijayo baada ya utekelezaji vipengere sita vya kufikia malengo ya mpango huo kukamilika.

Alisema vipengere vinavyotekelezwa kwa sasa ili kuwezesha kufikiwa kwa lengo hilo, ni pamoja na kazi ya kutambua asasi za kiraia zinazohusika na maendeleo ya vijana na kuzishirikisha katika mpango huo kwa kuziwezesha kutoa elimu ya kuamsha upeo wa vijana kuingia katika ujasiliamali wa ushindani.

Mpango huo utakakamilika na kupatikana ajira hizo itakuwa ni sehemu ya malengo ya Tume ya Maendeleo ya Afrika, unaolenga katika kukuza ajira kwa vijana na kupambana na umasikini kupitia sekta ya ujasiliamali katika nchi hizo.

Naye Ofisa wa elimu ya ushirikishi na mawasiliano wa YEF, Miriam Christensen alisema mpango huo utatekelezwa kwa miaka mitano kwa ufadhili wa awali wa dola za Marekani milioni 24 kutoka Shirika la Maendeleo ya Kimataifa la Denmark (DANIDA) na Tume ya Maendeleo ya Afrika.

Akizungumza kwa upande wake katika semina hiyo iliyofanyika Mji Mkongwe ambao ni Urithi wa Kimaaifa, Mratibu wa mpango huo kwa upande wa Tanzania, Mkuku Louis asasi za kiraia 27 kati yake 20 Tanzania bara na saba Zanzibar ambazo zinahusika na maendeleo ya vijana Tanzania bara na Zanzibar , zimechaguliwa hapa nchini baada ya kukidhi sifa za kushiriki katika utekelezaji wa mpango huo.

Louis alisema hatua ya kwanza ya utekelezaji wa mpango huo kwa upande wa Tanzania imekamilika kwa kutambua asasi za kuingia katika mpango na kazi inayofuata ni kutoa elimu kwa asasi hizo juu ya namna ya kuamsha upeo wa vijana kuingia katika ujasiliamali wa ushindikani na uzalishaji mali.

“Tumechagua maeneo hayo mawili kwa sababu hatutaki tuwe wasindikizaji tu au mnaonaje na nyinyi,” aliwauliza vijana hao Louis.

Alisema kwamba bila kuwapa vijana elimu katika ujasiliamali wa ushindani, Tanzania haitanufaika katika mpango huo kwa kiwango sawa na Kenya na Uganda kwa kuzingatia nchi hizo zimepiga hatua katika kutoa elimu ya ujasiriamali kwa vijana wake.

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s