Tumejivua gamba kweli

Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara, Pius Msekwa amesema chama chao kimezaliwa upya kwa mara ya pili kutokana na mabadiliko ya kujivua gamba yaliofanyika hivi karibuni.

Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara, Pius Msekwa amesema chama chao kimezaliwa upya kwa mara ya pili kutokana na mabadiliko ya kujivua gamba yaliofanyika hivi karibuni.

 Alisema mabadiliko hayo yameleta faraja kubwa na kurejesha imani kwa wanachama na wapenzi wa chama hicho kwani chama hicho awali kilizaliwa mwaka 1977 na sasa kimezaliwa tena kwa mara ya pili na kuwataka wananchi kurejesha imani kwa chama hicho na kuachana na kusikiliza maneno ambayo chama hicho huzaliwa kwamba ni chenye kukumbatia mafisadi na matajiri.

Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Bi Asha Abdallah Juma amesema hakuna chama chochote cha siasa chini Tanzania kitakachopewa kuongoza nchi zaidi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ambacho ndicho chenye uwezo huo.

Alisema lengo la chama hicho kujivua gamba ni kujipanga upya katika kuendeleza ushindi wa kawaida ambao chama cha mapibnduzi umekuwa ukishinda katika miaka yote katika chaguzi zake zinazofanyika nchini.

 “Lengo ni kuendeleza ushindi na hatuwezi kumpa chama chengine chochote kuongoza serikali isipokuwa CCM hakuna CUF wala mim wala nini hapa” alisema Kiongozi huyo ambaye alipanda jukwaa kwa kasi na kushangiriwa na wanachama waliofika kusikiliza mkutano huo.  

Ameyaeleza hayo wakati akihutubia mkutano wa hadhara uliofanyika katika viwanja vya Kisonge mara baada ya kupokelewa kutoka bandari ya Malindi wakitokea Jijini Dar es Salaam ambapo hivi karibuni viongozi hao waliteuliwa baada ya sekreteriet ya chama hicho kujiuzulu na kulazimika kuundwa upya.

Akizungumza katika mkutano huo Katibu Mwenezi wa CCM Nape Mosses Nnauye amesikitishwa na wanasiasa wenye kubeza uamuzi uliochukuliwa na chama chake wa kujivua gamba na kuwataka wanaobeza hatua hiyo wajaribu wao kufanya maamuzikamahayo katika vyama vyao.

Alisema uamuzi huo ni mgumu lakini ulilazimika kufanyika ambapo alisema ni sawa na mwenge ambao umewashwa Dodoma lakini mwenge huo utazunguka nchi nzima na kumurika katika maeneo yote ili kurejesha imani ya wananachi na wana CCM ambao kwa muda mrefu wamekata tamaa na chama chao ambacho kinazuliwa kuwa ni chama cha mafusadi na chama cha matajiri jambo ambalo halina ukweli.

Aliwaambia wanachama wa CCM Zanzibar warejeshe matumiani kwa chama chao lakni zaidi chama kimeamua kujisafisha na kuzaliwa upya hivyo wale wote wenye shutuma wajitose kabla haajatoshwa kwani wakichelewa watatoshwa kwa lazima ili boti iendelee na safari yake.

“Tunawaambia kabla boti yetu haijaondoka wale wote wanatuhumiwa ndani ya chama chetu tunataka watoke lakinikamahawataki basi tutawatosha kabisa ili sisi tuendelee na safari” alisema Nape na kushangiriwa.

Aidha alisema wapo watu wanaotumia magazeti, vyama vya siasa na viongozi wa dini kutaka kuwachafulia CCM kwa kisingizio cha kutokukubaliana na uamuzi wa kujivua gamba lakini ameahidi kwamba vita hiyo haitakwisha mara moja na kuwatahadharisha kuacha mara moja tabia hiyo kabla ya kuripuliwa.

“Tunajua wapo ambao wanatumia vyombo vya habari, vyama vya siasa, viongozi wa dini kutaka kutuchagua lakini sisi tunasema wasijaribu maana vita hii haitaisha na tunawaahidi kamwe hawatashinda …tunawaambia wasirushe mawe katika nyumba ya vigae” alisema Nape kabla ya kushuka jukwaani ambapo alipanda kwa ajili ya kutambulishwa.

Alisema lengo la kutolewa miezi mitatu kwa wale wanaotuhumiwa kujiondoa katika chama ni sawa na pweza unapotaka kumla lazima umpige na michanga hivyo katika miezi hiyo mitatu n kujisafisha kabla ya kuliwa.

Akizungumza katika mkutano huo Januari Makamba amesema chama cha Mapinduzi hivi sasa kitaendeshwa kisiasa na lengo ni kuelekea katika uchaguzi mkuu ambapo chama kimepata watu wataalamu na wenye kufanya mipango yake kitaalamu zaidi kuliko kilivyokuwa mwanzo hivyo hakuna sabbau ya vijana kuvunjika moyo hasa kwa kuzingatia vijana ndio waliopewa majukumu ya kuendesha chama.

“Hatutaki kusemasanamaana tunaendesha kitaalamu zaidi na mtendaji mzuri ni yule anayesema kidogo na kutendasanavitendo vyetu mtaviona wakati wa uchaguzi tutajipanga vizuri mambo yetu na tutakiletea ushindi mkubwa cama chetu sasa wanachama mrejeshe matumaini katika chama chetu na kuleta umoja na mshikamano” alisema Makamba.

Akitoa salamu zake za shukrani Vuai Ali Vuai ambaye ni Naibu Katibu Mkuu wa CCMZanzibaralisema lengo ya kuchaguliwa yeye ni kukiunganisha chama cha mapinduziZanzibarna kukiimarisha hivyo aliwataka wanachama wanaokwenda kwake wapeleke maneno yenye kujenga chama na kukataa fitna na majungu kupelekewa ofisini kwake.

“Rafiki yangu ni yule atakayekuja kuzungumzia namna ya kukiimarisha chama chetu lakini yule anaekuja ofisini kwangu na maneno ya kuwa eti fulani sio mtu mzuri usishirikiane naye huyo sitamkaribisha ofisini kwangu fitina na majungu sitaki nataka kuunganisha chama ili chama chetu kiendelee kuleta ushindi wa kishindo” alisema Vuai.

Akitoa historia refu na kutaja sababu zilizoifanya CCM kujivua gamba, Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara, Pius Msekwa alisema lengo ni kukiweka sawa chama lakini sasa kimeshakaa sawa na kuwaomba wananchi kuridhika na uamuzi huo mgumu ambao chama chengine chochote kisingeweza kuiga mfano huo.

Alisema CCM ndio inayobebeshwa mzigo wa kuambiwa na vyama vya upinzani kwamba CCM ni mafisadi na chama cha matajiri jambo ambalo halina ukweli hivyo alisema CCM wajue kwamba chama kimezaliwa upya na hakuna mchezo bali ni kujitayarisha na uchaguzi ili heshima na nidhamu ya chama irudi miongoni mwa wapenzi wa chama hicho na wana CCM.

Advertisements

One response to “Tumejivua gamba kweli

  1. mimi munanichekesha sana sana unawambiya watu waziwazi kuwa mumejivuwa gamba kwahiyo munajuwa fika kuwa miaka yote hii mumewasaliti watanzania na ss ndio munajirekebisha kisha unasema ilikuwa nitabu sana kukibadilisha chama ila ss mushakibadilisha na kiko safi njee si ni nyinyi kwa nyinyi mbona hatuoni sura mpya??? kisha umesimama hapo unawambiya wanachi kuwa mujipange kwa uchanguzi ujao nimiaka mingapi mpaka uchanguzi tayari unapiga kelele husemi kuwa ss tutawashughikiya wanchi wapate maji kwenye nyumba zao bila ya kuteka kwa ndoo na madumu husemi wala husemi umeme utawekwa sawa ila watu wawe na umeme husemi wala husemi tutahakikisha vijana wote wanaofeli darasa la saba watafundishwa kazi za mikono ili waweze kujisaidiya husemi wala husemi kuwa tutahakikisha watu wote watakuwa na maisha mazuri yani kila mtu awezekupata kula na mahali pa kuishi vizuri husemi ww booooooooom unafikiria uchanguzi ili uhakikishe kuwa kula yako na watoto wako iko poa ila wanaokupa kura poteleyambali wache wafee na njaa sasa hilo gamba unalolotaja umelivuwa ni gamba ngani??????kisha unatisha watu kama wandishi wa habari na waumini wa dini kuwa wasijaribu kusundio lako nini ww kuwatisha ww ni kiongozi wa chama kama watu hawakukuchanguwa inamaana hawakutaki ss ikiwa ww unawatisha basi ww sio kiongozi bora ww ni DIKTETA ndio wanaolazimisha watu wawapende hatakama hawawataki MFANO MZURI GADDAFI wanchi waliyo wengi washamkata lakini bado anaghanganiya ss nawewe kama watu hawakukuchanguwa UTAWAUWA KAMA ANAVYO FANYA GADDAFIII?????????

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s