Buriani Bi Rahma

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein,akitia udongo katika kaburi la Marehemu Rahma Mshangama,aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Ustawi wa jamii,maendeleo ya Vijana Wanawake na Watoto,aliyezikwa leo katika makaburi ya Mwanakwerekwe Mjini Unguja.

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein leo ameungana na viongozi mbali mbali pamoja na wafiwa na wananchi  katika mazishi ya Katibu Mkuu Wizara ya Ustawi wa Jamii na Maendeleo ya Vijana Wanawake na Watoto Marehemu Bi Rahma Mohammed Mshangama.  

Katika mazishi hayo pia, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Mohammed Kharib Bilal alihudhuria pamoja na viongozi wengine wa serikali, vyama vya siasa, dini na wananchi mbali mbali.

Mapema mara baada ya Salat Jumaa, maiti ya Maremu Bi Rahma Mshangama ilisaliwa katika msikiti wa Ijumaa Mwembeshauri, mjini Unguja na baada ya hapo ilienda kuzikwa katika makaburi ya Mwanakwereke nje kidogo ya mji wa Zanzibar.

Bi Rahma Mshangama  alifariki jana  katika hospitali ya MnaziMmoja mjini Zanzibar, Marehehemu Bi Ramha alizaliwa tarehe 21 Aprili 1961 Kikwajuni Mjini Zanzibar na kupata elimu yake ya msingi  mwaka 1969 mpaka 1978 katika skuli ya msingi na Sekondari ya Kidutani na Lumumba Zanzibar.

Mnamo mwaka 1979 mpaka 1981 alipata elimu ya Juu katika Chuo Cha Lumumba ambapo katika mwaka huo wa 1981 aliajiriwa katika Wizara ya Kilimo na Maendeleo ya Mifugo.

Mwaka 1985 mpaka 1987  alipata elimu ya Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine, Mkoani Morogoro ambapo mwaka 1991 alihudhuria mafunzo ya Utafiti wa Masuala ya Elimu na Ufugaji katika Chuo Cha Mifugo Afrika nchini Ethiopia.

Mwaka 1989-1990 alihudhuria mafunzo ya (MSC) Uzalishaji wa  wanyama katika Chuo cha Reding University nchini Uingereza na mwaka 1991 alihudhuria mafunzo ya Ukuzaji Kilimo pamoja na Mafunzo ya Maendeleo ya Wanawake katika Kilimo nchini Uingereza na mwaka 1996 alihudhuria mafunzo ya Ubinafsishaji nchini Ireland.

Katika uhai wake Marehemu Bi Rahma Mshangama aliwahi kuwa Mjumbe wa Bodi ya Shirika la Posta kuanzia mwaka 1996, na pia alikuwa Mjumbe wa Bodi ya Uzalishaji wa wanyama nchini Tanzania kuanzia mwaka 1989 mpaka alipofariki.

Kwa upande wa nafasi alizowahi kushika Marehemu Bi Rahma Mshangama aliwahi kuwa Mkuu wa Idara ya Mifugo katika kitengo cha Mifugo mnamo mwaka 1987-1989, mwaka 1991 hadi 1992 alikuwa Mkuu wa Kitengo cha Kamisheni ya Mashamba ya Serikali katika Wizara ya Kilimo na Mifugo.

Mwaka 1992 hadi mwaka 1995 alikwua msaididi wa Meneja wa Mradi wa Mpango wa Chakula wa Umoja wa Mataifa hapa Zanzibar na mwaka 1995 hadi mwaka 2000 alikuwa Katibu Mkuu Wizara ya Wanawake na Watoto na mwaka 2000 hadi 2008 alikuwa Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Maliasili na Ushirika na mwaka 2008 hadi 2010 alikuwa Katibu Mkuu Wizara ya Kazi Maendeleo ya Vijana Wanawake na Watoto.

Hadi anafariki Bi Rahma Mshangama  alikuwa  Katibu Mkuu Wizara ya Ustawi wa Jamii na Maendeleo ya Vijana Wanawake na Watoto. Bi Rahma Mshangama ameacha mume na Mama Mzazi.

Mapema katika hotuba ya Sala ya Ijumaa, akieleza sifa za Marehemu Bi Rahma Mshangama, Sheikh Fadhil Soraga alisema kuwa Bi Ramha Mshangama atakumbukwa  daima kutokana na alikuwa mchapa kazi hodari na aliishi na jamii kwa wema mkubwa  na kumuombea  kwa Mwenyezi Mungu amuweke mahala pema peponi, Amin.

  

Advertisements

One response to “Buriani Bi Rahma

  1. S/A NATOWA POLE ZANGU KWA JAMAA NA MARAFIKI WA BI RAHMA ILA PIA NATAKA KUWAKUBUSHA KUWA LEO NI BI RAHMA KESHO NI MIMI AU WEWE je mumeona hiyo nyumba tutakayo ishii miaka isiyojulikana mpaka siku ya KIYAMA ifiki wakati wa kuhukumiwa na M/MUNGU je viongozi muliyobakiya hai na majumba mnayojijengeya na magari mazuri mazuri munayojinunuliya nyinyi na familiya zenu je mutakwenda nayo huko mbele ya haki??kama laaaaa basi haina haja ya kujirundikiya mali na majumba na mashamba maana huwende navyo kaburini utaviwacha hapa hapa duniani nyinyi kama viongozi mapesaya na mashamba muliyojerundikiya wapeni wanchi waliyo masikini ambao ndio wanaokuchaguweni hawana hata vitanda hawana hata bofulo na kunywa na chai hawana hata maji ya kuoga na nyinyi munajuwa yote hayo ila hamusemi mumo tu kujirundikiya mamali na mashamba na majumba mazuri ila sote mwisho wetu ni kama marehemu BI RAHMA tafakarini kabla hamujafa maswahaba walimuliza mtume muhammed s.a.w nani ataingia peponi mapema akasema masikini na nani atachelewa kuingia peponi akasema tajiri je habu jiulize kweli unataka uchelewe kuingia katika pepo ya?????? ALLAH ikiwa tumejaliwa kuingia maana kuna mambo kibao mbali na hayo ya kujirundikiya mamali ambayo tumefanya kenyuma na ALLAH alivyosema.TAFAKARI KABLA YA ATHARI.
    M/MUNGU AMLAZE PEMA PEPONI BI RAHMA

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s