Choma moto rasimu

Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Demokrasia Maendeleo Zanzibar (CHADEMA) Hamad Mussa Yussuf na akiwaonesha wananchi rasimu ya mswaada wa katiba ambayo chama hicho kiliuwasha moto baada ya kusema haukubaliki na una kasoro nyingi hivyo haupaswi kuendelea kujadiliwa

CHAMA Cha Demokrasia na Maendeleo Zanzibar (CHADEMA) kimeichoma moto rasimu ya mswada wa uandaaji wa katiba mpya ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania hadharani kuashirikia kutokukubaliana na rasimu hiyona kumtaka Rais wa Zanzibar kuitisha kura ya maoni kuukataa Muungano.

Tukio hilo la kuchomwa moto rasimu hiyo ya katiba imefanyika juzi katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika viwanja vya Kibanda Maiti baada ya viongozi wa chama hicho kuwaleza mapungufu ya mswada huo na kutokukubaliana nao ambapo walisema uchomaji moto ni ishara ya kuonesha viongozi wa serikali kwamba wana Chadema wa Zanzibar hawakubaliani ya rasimu hiyo ya mswaada.

Naibu Katibu Mkuu wa Chadema Zanzibar, Hamadi Mussa Yussuf aliwataka viongozi wenzake kusogea na kuiwasha rasimu hiyo huku akiwataka wananchi kushangiria kwa nyimbo maalumu za chama hicho za kukpongeza chama hicho kwamba ni kiboko ya mafusani nchini.

“Hatukubaliani na rasimu hii na ili kuonesha hasira zetu na kuonesha kwamba hatuna imani na rasimu hii ya katiba na haina manufaa na tija kwetu tunaichoma moto ili serikali nayo ione kwamba hii nio rasimu ya katiba inayotakiwa na wazanzibari” alisema Yussuf.

Yussuf alisema anamuomba sana Rais wa Zanzibar kuitisha kura ya maoni kwa waanzibari kuukataa muungano kwa kuwa hauna manufaa kwao.

“Tunamuomba sana Rais wa Zanzibar Dk Ali Mohammed Shein aitishe kura ya maoni kuukataa muungano maana tumechoka kuona utitiri wa kero za mungano ambazo zinazungumzwa tu bila ya kupatiwa ufumbuzi” alisema Kiongozi huyo huku akishangirwa na wananchi na wanachama kadhaa waliofika uwanjani hapo.

Aidha aliomba Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kutokubali kupokea rushwa katika kushawishi kuikubali rasimu hiyo ya katiba mpya ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kusema kwamba chadema inashukuru kwamba imepokea rasimu ambayo ni kiini macho kwa wananchi.

Alisema rasimu hiyo iliyoletwa Zanzibar na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania hakuna yeyote atakaekubali kwa kuwa haitakii mema Zanzibar na zaidi imekuwa ikiinyima Zanzibar fursa kutokana na kuwa imeidharau kama ni nchi na kuwa ina hadhi sawa na Tanganyika.

Akizungumza katika mkutano huo ambayo uliwashikisha baadhi ya vyama vya NCCR-Mageuzi, Ali Omar Juma alisema hakuna rasimu ya katiba inayoandikwa bila ya kuzingatia umuhimu wa Zanzibar na hadhi yake hivyo wananchi hawana imani na mswaada huo na kuahidi kwamba watatumia kila njia kuipinga rasimu hiyo nchi nzima.

Alisema wametoa maoni yao kuipinga na baadae wataitisha maandamano makubwa ya amani kwa nchi nzima kuipinga ili isipelekwe bungeni kwa kutokana na rasimu hiyo haijazingatia mambo muhimu huku suala la Zanzibar likiwa limeachwa nyuma katika utayarishaji rasimu hiyo.

“Tuaitisha maandamano makubwa sana lakini ni maandamano ya amani na tutaitisha maandamano hayo kwa kuwashawishi wananchi waikatae rasimu hii ya katiba ambayo haina faida wala maslahi ya wananchi wa Zanzibar….kwa hivyo sisi tutaipinga moja kwa moja na tunakuombeni wananchi mtuunge mkono katika hili” alitoa wito kiongozi huyo katika mkutano ambao haukuwa na watu wengi katika kawaida ya mikutano wa CCM na CUF hapa Zanzibar

Juma alisema wanchi wa Zanzibar tayari wameshapeleka notisi kwa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN) Ban Ki Moon kutoikubali rasimu hiyo na wanachosubiri ni majibu kutoka UN ili waipeleke mahakamani serikali kwa kufanya mambo na kuikiuka misingi ya kisheria za kimataifa.

Alisema wananchi wa Zanzibar wako tayari kuishitaki Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika mahkama ya kimataifa iwapo itapitisha mswada huo wa katiba mpya na kuwasisitiza wananchi kuuna mkono hatua zote za harakati hizo ambazo zimeanza kuendelea nchini.

Kwa upande wake Makamu Mwenyekiti wa Chadema Zanzibar, Said Issa Kassim alisema bunge la jamhuri ya muungano wa Tanzania limekuwa likitunga sheria za kuwakandamiza wazanzibari huku waziri wa Afrika Mashariki Samweli Sitta akiwa ni shuhuda wa masuala hayo.

Alisema Waziri Sitta ndiye aliyeongoza Bungeni kupitisha uamuzi wa rais wa Zanzibar kuondoshwa kuwa Makamo wa pili wa rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika kipindi alichokuwa waziri wa sheria na ameshangazwa mtu huyo huyo anakubali kutumwa kuja kuwaletea wazanzibari rasimu ya mswaada watu ambao wamewakandamiza katika bunge lake.

Alisema mabadiliko ya 11 ya katiba ya Jamhuri ya Muungno wa Tanzania ndio yaliyopelekea rais wa Zanzibar kupoteza nafasi kuwa Makamo wa rais wa Tanzania ambayo ilipitishwa na Waziri Sitta bungeni akiwa Waziri wa sheria wa Jamhuri ya Muungano na kamwe wazanzibari hawatasahau suala hilo.

Muasisi wa kampeni ya washa taa mchana, Grayson Nyakarungu aliwataka wananchi kuendeleza mapambano na kamwe wasirudishwe nyuma na mafisadi kwani lengo la kuwasha taa hizo ni kumurika na kutoa alimu kwa wananchi juu ya vitendo vinavyoanywa na mafisadi nchini.

Mdadala wa wa siku mbili wa kutoa maoni kuhusu mswaada wa kuundwa kwa kamisheni ya kukusanya maoni kuhusu kutungwa kwa katiba mpya ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania awali ulikwenda vizuri kwa siku ya mwanza lakini siku ya pili ulishindwa kuendelea baada ya wananchi kuhamasika na kuukatisha kwa kuichanachana rasimu ya katiba hiyo iliyokuwa ikitolewa maoni ya wadau mbali mbali ambapo mkutano huo ulivunjika.

Kiongozi wa Jumuiya ya Maimamu Zanzibar (JUMAZA) Sheikh Farid Hadi Ahmed alikuwa wa kwanza kutoa maoni yake ambayo yalionesha kwamba rasimu hiyo haifai kujadiliwa na kuwauliza wananchi kama wanaitaka au hawaitaki na baadae kuichana chana akisema kitendo hicho ni kufikisha ujumbe kwa serikali kwamba wazanzibari hawataki tena kuonewa na kutungiwa vitu ambavyo haina faida wala manufaa navyo.

Advertisements

One response to “Choma moto rasimu

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s