Vijana wajikosha kwa wazee

Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) wakiwa katika tayari kwa ajili ya matembezi ya kumuezi Marehemu Mzee Abeid Amani Karume katika kabla ya maadhimisho ya kifo chake, Vijana hao wamesema kutoa matamshi juu ya chama chao wasionekane kuwa wanamlenga mtu au kiongozi bali wanatimiza wajibu wao kama vijana na kamwe hawatanyamazishwa na kiongozi yeyote katika harakati hizo za kukijenga chama chao

UMOJA wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) umesema kamwe hawataweza kunyamazishwa na viongozi au kikundi cha watu wachache wenye dhana mbaya kwa madai ya kuwa vijana wa sasa hawaheshimu wazee hoja ambayo kwa sasa imekuwa ikilaumiwa kwa vijana.Mwenyekiti wa UVCCM, Beno Malisa akitoa saalamu zake katika matembezi ya kumbukumbu ya matembezi ya kumuenzi Marehemu Mzee Abeid Amani Karume aliyewahi kuwa Rais wa kwanza wa Zanzibar, alisema Umoja wa Vijana hautaweza kunyamazishwa na viongozi ambao wanajenga dhana kuwa umoja huo hauwezi kuwakosoa wazee.
Vijana haop wamesema kumekuwepo dhana kwamba vijana unapofanya hivyo ni wanaonekana wametumwa na wanasiasa au wanambeba kiongozi fulani jambo ambalo sio la kweli.Malisa alisema hiyo ni dhana potofu ya kuiona Jumuiya hiyo kuwa haiwaheshimu wazee jambo ambalo linapaswa kufutwa kwa baadhi ya viongozi kwani bado wanaheshimu wazee na wanalinda heshima zao ndani ya chama cha Mapinduzi na sio kweli kama wanatumwa.
“Nasema haya kwa uchungu kabisa hii dhana ya kwamba vijana wa sasa hatuheshimu wazee au tunatumiwa na watu ni dhana mbovu kabisa na dhana usiyo na mashiko kwa sababu sio jambo la kweli sisi tutaendelea kukosoa na kusema pale ambapo kuna kasoro” alisema kiongozi huyo.
Alisema kwa kuzingatia hayo ndio maana huamua kutumia vikao vya Baraza Kuu la UVCCM kuweza kutoa maazimio yao ambayo yanahitaji kuheshimiwa kwani ni moja ya utaratibu wa chama na ni wakawaida.
“kuanzia sasa viongozi wanaojenga dhana hiyo wasifikirie kuwa wataweza kutusimamisha sisi vijana lakini tunaahidi tutaendelea kuwa wakali kama pilipili na moto wetu hautazimwa kamwe”. Alisisitiza huku akiungwa mkono na vijana wenzake kwa kupigiwa makofi mengi.Kiongozi huyo alisema dhana ya CCM katika kuendeleza chama ni kuona wanasema kweli daima na fitina kwa Umoja huo zitakuwa ni mwiko kwao kwani wanachukizwa na vitendo vya ufisadi na ubadhirifu wa mali za umma.
Akiongea katika mkutano huo ambao umefanyika Afisi Kuu ya CCM Kisiwandua Naibu wa Umoja huo Zanzibar Jaffar Kassim Ali, akitoa salamu zake alisema kwa kiasi kikubwa matembezi hayo yameweza kufanikiwa kwa kuweza kutoa elimu mbali mbali ikiwemo ya ukimwi, historia ya Zanzibar na dawa za kulevya kwa vijana hao.
Alisema kuwa wanachojiandaa hivi sasa ni kuona wanajipanga kwa kutafuta viongozi wazuri ambao wataweza kukivusha chama hicho vuguvugu linaloendelea na kukituliza chama chao kiendelee na mikakati yake ya utulivu na kupata wanachama wengi zaidi.
Akitoa salamu zake za kuwashukuru vijana hao na kuwapongeza kwa kuamua kufanya amtembezi hayo Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein vijana wanapaswa kulizingatia busara za viongozi wao waliotangulia.Alisema vijana ndio wataokuwa viongozi wa taifa la kesho ambalo linahitaji kuwapatia maendeleo wananchi wake na haitapendezesha wakaenda kinyume na misingi ya maisha ya Mzee Karume ambapo alichukizwa na wachache kunufaika na rasiliamali za nchi.
Dk Shein aliyasema hayo jana wakati akihutubia vijana 100 walioshiriki matembezi ya kumuenzi kiongozi huyo katika viwanja vya afisi kuu ya CCM Zanzibar.
Dk. Shein alisema ili kumuenzi marehemu Mzee Karume ni lazima vijana wachukizwe na vitendo vya ubadhirifu wa mali za umma kwani ni njia ya msingi katika kuiga maisha wakati wa uhai wake.Dk Shein alisema dhana ya Rais Karume kujenga tabia ya kuchukia ubadhirifu aliijenga kwa lengo la kuona uongozi wake unawanufaisha Wazanzibari kuwa na hali bora za maisha.

Kutokana na dhamira hiyo ya Rais Karume aliamua kutumia uhai wake kuhangaika pembe za dunia na Afrika kutafuta uongozi ambapo alifanikiwa na kuweza kujenga maisha ya Wazanzibari ambayo hayakuwa na ubaguzi wa aina yoyote.Alisema hali hiyo inahitaji kuendelezwa kwa kuona kila kijana anashiriki katika kuijenga nchi na ni lazima waone kuwa wanatumia misingi walioachiwa hasa ikizingatiwa ari waliyoianzisha UVCCM itaweza kufanikiwa.

Alisema hilo ni moja ya jambo la kuzingatia kutokana na serikali iliopo madarakani inahitaji kuona Zanzibar inakuwa ni yenye maendeleo chini ya ilani ya CCM ambayo serikali itajitahidi kuona inatekelezeka.Alisema jambo la msingi ambalo litahitajika kuona kuwa viongozi wa UVCCM, Jumuiya ya UWT na Jumuiya Wazazi zinaungana kufanya kazi pamoja ili kuhakikisha ilani ya CCM inatekelezeka.

Shein aliwataka viongozi wa UVCCM kujipanga vyema kuhakikisha CCM inakuwa na viongozi wazuri katika uchaguzi wa Chama 2012 kwani hao ndio chama itayowatumia kupata viongozi wa kukipatia ushindi chama katika uchaguzi wa 2015.Alisema ni lazima waanze kujipanga hivi sasa kwani CCM inachohitaji ni ushindi na katika uchaguzi huo wajue kuwa chama hakitatuma mtoto.

Ili kufanikisha hilo Dk. Shein aliwataka wanachama hao wa CCM kuendeleza amani nchini kwa kujenga misingi ya kupendana Jumuiya zote za Chama pamoja na Wazanzibari.Alisema tayari hivi sasa serikali imeanza kutekeleza mambo mbali mbali ambayo yatahitaji kupata nguvu za vijana na kuwepo kwa umoja wao ndio nguzo kuu ya kuweza kufanikisha hayo.

Mapema Dk. Shein katika matembezi hayo aliwapatia vyeti washiriki wote wa matembezi hayo akiwemo Mke wa Makamu wa Pili wa Rais Mama Asha Seif Iddi ikiwa ni hatua ya kuweza kutoa mchango mkubwa wa kufanikisha matembezi hayo.Maadhimisho hayo yalihudhuriwa na viongozi mbali mbali wa serikali akiwemo Makamu wa Pili wa Rais, Balozi Seif Ali Iddi na wanachama wa CCM ambapo matembezi hayo yaliweza kutembea katika Mkoa wa Kusini Unguja, Kaskazini na Mjini.

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s