Taratibu hazikufuatwa

Katibu Mkuu wa Afisi ya Makamu wa kwanza wa Rais Zanzibar, Dk Omar Dadi Shajaak alisema taratibu hazikufuatwa hivyo mswaada huo haukubaliki

Katibu Mkuu kutoka Ofisi ya Makamu wa kwanza wa Rais Zanzibar Dk Omar Dadi Shajak alisema Zanzibar si share holder, partner. Alisema kifungu kisomeke in agreement with Zanzibar president. Na Popote panapotajwa mwanasheria mkuu AG waende wote wawili na sio mwansheria mmoja tu. Ikiwa waziri waende wawiili lazima kuwe na Equal suiting. Kama ni two third iwe ya kila upande bungeni na baraza la wawakilishi. Bench mark ya referendum ni idadi gani iliyo registered au ipi?

Shajak alisema kwa kuwa utaratibu haukufuatwa basi mswaada huo haufai kabisa.”Taratibu za hazikufuatwa na misingi ya kujadil kama Jamhuri ya Muungano mswada huu ulifanywa kama miswada mengine inavyotengenezwa mchakato wa mswada huu haukubaliki kwani utaratibu haukufuatwa”.alisema Shajak.
Alisema mswada huo uko upande mmoja umepitishwa bungeni bila kuzingatia pande mbili zilizounda jamhuri ya muungano wa tanzania jambo ambalo haliwezi kuachiwa kupita hivyo hivyo kwnai kufanya hivyo ni kuidharau zanzibar ambayo ni mshirika kamili katika muungano huo wa nchi mbili huru.
“Mswaada huu wote urejeshwe bungeni na utengenezwe tena kama kwa kuweka usawa au vyenginevyo lakini kwa hivi haukubaliki kabisa” alisema Shajak.
Alisema lazima kuwe na makubaliano ya pande mbili huku akihoji itakuwaje pande moja isishirikishwe katika kutengeneza muswada huo na upande wa pili kuachwa kutoshirikishwa wakati nchi ndio zenye kupitishwa mwaada huo.
Alisema katika kasoro zake sekretarieti imechaguliwa kutoka upande mmoja hata kwa upande wa Zanzibar hakushirikishwa ni vyema kukawa na usawa ili kushirikishwa Wazanzibari.
Shajak alisema kwamba katika Bunge jambo linalohusu katiba ya Zanzibar na suala lolote lile la Muungano ni vyema kutumika usawa wa wajumbe Zanzibar na Tanganyika na sio kuamuliwa tu na wajumbe kutoka upande wa tanzania bara peke yao.

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s