Spirit ile ya Jumbe bado ipo

Mzee Hassan Nassor Moyo ni miongoni mwa waasisi wa Muungano na pia ni muasisi wa Maridhiano haya yaliopo ambaye wakati wa makubaliano ya Muungano wa Zanzibar na Tanganyika alikuwa waziri. wa sheria .“Nilikuwa waziri wa sheria wakati huo mambo haya yalikuwa 11 na ushahidi huu hapa lakini hivi sasa yameongezeka naambiwa yamefikia zaidi ya 30 haya yote yaliongezwa na wenzetu bara ...na kwa yale yaliyoengezwa na watu wa Unguja, Jumbe alifukuzwa kazi sasa kwa hayo hayo sasa Spirit ile ile ya Jumbe ipo bado maana sisi wengine tuhai hatujafa na yeye pia yupo hajafa na wengine pia wapo wahai ambao wanaunga mkono. Wananchi wasikilizwe wanataka Muungano gani wataamua waachiwe wenyewe tusiwadharau hawa”

Akiongea katika mjadala huo Mzee Nassor Moyo ambaye alikuwa waziri wa sheria wakati muungano uliopoundwa alisema yeye amekuwa shahidi wa makubaliano hayo kati ya Zanzibar na Tanganyika.

“Nilikuwa waziri wa sheria wakati huo mambo haya ni 11 lakini hivi sasa yameongezeka naambiwa yamefikia mpaka 30 haya yote yaliongezwa na wenzetu bara ….na kwa yale yalioengezwa na watu wa unguja Jumbe alifukuzwa kazi sasa spirit ile ile ya Jumbe ipo maana sisi wengine tuhai hatujafa na pia wapo wanaunga mkono na yeye mwenyewe jumbe hajafa yuhai””alisema Mzee moyo huku akionesha nakala ya makubaliano hayo ya muungano.

Alisema mambo waliokuwa wameafikiana Nyerere na Mzee Karume wakati huo yameweza kuheshimiwa na viongozi wengine kulingana na wakati lakini kwa sasa vijana hawawezi kupangiwa mambo kama ilivyokuwa huko nyuma ambapo sas vijana wanahitaji kurekebisha na kuwepo muundo wanaoutaka wao jambo ambalo alisema lazima serikali iwasikilize wananchi.

“Tusiwazuwie vijana hawa kufanya muungano wanaoutaka wao wenyewe, mimi na karume na jumbe tumeufikisha hapa …na haiwezekani kama tumeshaufikisha hapa halafu tuendelee hivi hivi bila ya wao vijana kuwaachia wenyewe wanavyotaka kuuendeleza lazima tukubali kuwapa fursa waseme wenyewe wanataka muungano wa iana gani …tusiwazuwia wenyewe …sisi yetu tumeshwikwisha” alisema Mzee Moyo.

Mzee moyo alisikitishwa na tabia ya kuambiwa kwamba suala la muungano zilijadiliwe jambo ambalo amesema iwapo halitazungumzwa kutakuwa hakuna jembo jengine la kulijadilia zaidi ya muungano kwa kuwa ndio kubwa kwa Zanzibar.

“Mnatwambia tusizungumze suala la muungano mnataka tuzungumze nini hapa wakati hilo ndio jambo la msingi….mnataka tuzungumze nini …hili ndio jambo tutakalolizuingumza” alisema huku akisisitiza kwamba kosa walilolifanya wakati huo hivi sasa lisirudiwe tena kwa kuwa vijana wa sasa wamesoma na sio wajinga kama wao ambapo haifai kupuuzwa vijana hao.

Akizungumza katika mjadala huo, Waziri wa Katiba na Sheria, Abubakar Khamis Bakari alisema utaratibu uliotumiwa sio na serikali haikushirikishwa katika uandaaji wa rasimu hiyo na serikali ya muungano haifajafan ya uungwana hata kidogo.

Alisema licha ya kuwa hawajashirikishwa lakini serikali ya Zanzibar kupitia mwanasheria mkuu wake aliandika barua kupeleka serikali ya muungano lakini hakujibiwa angaua kwamba barua yao imepokelewa lakini pia walipeleka mapendekezo yao 14 lakini jambo la kusikitisha ni mambo mawili tu ndio yalioingizwa katika rasimu hiyo na badala yake kuongezwa mambo mengine manane kinyume na makubaliano.

Advertisements

One response to “Spirit ile ya Jumbe bado ipo

  1. Aslam aleikum,
    Pongezi Wazanzibar na viogozi hivi ndivyo tunavyotaka viongozi wa Zanzibar wasijali chama waijali Zanzibar inapozungumza Zanzibar ni yawote pongezi tena kwa umoja wenu na msimamo wa viongozi na wananchi.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s