Mabadiliko ya 10 yamewagusa

Mwanasheria Mkuu wa serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Othman Masoud Othman alisema ni kweli marekebisho ya 10 ya katiba ya Zanzibar yamegusa Muungano ingawa katika katiba hiyo kifungu cha 17 kimempa uwezo rais wa Zanzibar kuwa na uhuru wa kuteuwa wakuu wa mikoa na kukata mipaka ya mikoa bila ya kushauriana na rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania jambo ambalo Zanzibar wamerekebisha huku akihoji jee kufnaya hivyo kurekebisha makosa ni ni vibaya au ni kosa hata wengine hawamaki?.

Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Othman Masoud Othman alisema …marekebisho ya kumi yamegusa katiba ya muungano. Zanzibar kurekebisha makosa imekuwa ni kosa? Bunge halina uwezo kutunga ya sheria ya kuweza kutunga katiba nyengine. Articles of the union ndio iliyozaa katiba hii ya muungano. Turudi katika mapatano ya muungano, tushauriane na tukubalinae. Madaraka hayo yametoka wapi ndani ya katiba hii?

Bunge la jamhuri halina uwezo wa kutunga sheria ya katiba hili ni jambo la msingi si dhani Zanziba na watu wake kama watakubali kuvunja katiba.
Wakitoa maoni yao wazanzibari leo wameukataa mswaada wa kuundwa kwa kamisheni ya kukusanya maoni kuhusu kutungwa katiba mpya ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Visiwani Zanzibar kwa madai kwamba serikali ya Mapinduzi Zanzibar haijashirikishwa katika uandaaji.
Wazanzibari hao wamesema suala la kutengenezwa mswaada wa kuundwa katiba mpya ya Tanzania limefayika bila ya kuzingatia upande wa Zanzibar ambao ni mshirika wake muhimu wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania.
Wananchi hao wamesema utaratibu uliiotumika katika mswaada wa katiba mpya haukuwashirikisha wanzibari na badala yake umefanyika kwa upande mmoja wa jamhuri ya muungano wa Tanzania jambo ambalo sio sahihi kwa kuwa bila ya kuwepo Zanzibar kusingekuwepo na Tanzania.
Maoni hayo yametolewa jana na wananchi mbali mbali wakiwemo mawaziri, makatibu wakuu, viongozi wa dini na wananchi mbali mbali katika mdahalo wa wazi wa kukusanya maoni katika ukumbi wa Hoteli ya Bwawani Mjini Zanzibar juu ya utoaji wa maoni ya kuhusu mswaada wa kuundwa kwa kamisheni ya kukusanya maoni kuhusu kutungwa kwa katiba mpya ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Zanzibar.
Akichangia mjdala huo Mwakilishi wa Jimbo la kwamtipura Hamza Hassan Juma amesema mswada wa marekebisho ya katiba ya Muungano una mapungufu mengi yakiwemo kutoshirikishwa kwa serikali ya Zanzibar.
Hamza alifahamisha kuwa Serikali ya Zanzibar haikushirikishwa kikamilifu ili kutoa maoni yake na wala haukupelekwa katika baraza la wawakilishi kupata maoni ya baraza hivyo haukustahiki kupelekwa Bungeni kujadiliwa kwani umekosa ridhaa za pande mbili.
“Mswada huo ni vyema kurudi Serikalini na ukafanyiwe marekebisho na badala yake upelekwe katika Baraza la Wawakilsihi ili kujadiliwa ili upate ridhaa ya nchi mbili zilizoungana”alisema Mwakilishi Hamza.
Kwa upande wake mjumbe kutoka chama cha mapinduzi (CCM) Ali Mwinyi Msuko alisema wanasheria wa Zanzibar wakae na wanasheria wa Tanzania bara kuupitia upya mswada huo na hakuna sababu ya kuharakisha muswada huo kwenda bungeni rais Nyerere na Karume walikubaliana katika Muungao huo na kwa sasa nchi mbili hizi zikubaliane.
Alishauri kwamba mswada huo urudi tena Bungeni na ufuate taratibu kwa kisheria na kwa sasa hakuna sababu yeyote ya kujadiliwa huku akitoa mfano kwamba kujadili mswada huo ni sawa na kutwanga maji kinuni. Na mswaada huo haukuzingatia hali halisi ya Zanzibar…vipi ifanyike ijumaa wakati 98% ni Waislamu wanataka kusali? Hauna haja ya kurakishwa kupelekwa June.

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s