SMZ yagoma kuilipa TANESCO

Waziri wa Ardhi, Maji, Makazi na Nishati wa Zanzibar, Ali Juma Shamhuna na Mwakilishi wa Jimbo la Donge Kaskazini Unguja aliwaeleza wajumbe wa baraza la wawakilishi kwamba kamwe SMZ haitolipa fedha kwa Shirika la Umeme Tanzani (TANESCO)

 

SERIKALI ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) imekataa kulipa deni la umeme la shilingi bilioni 40 kwa TANESCO baada ya kupandishiwa kiwango cha malipo.

 Waziri wa Ardhi, Maji, Makazi na Nishati wa Zanzibar, Ali Juma Shamhuna amesema baada ya kiwango serikali ya Mapinduzi Zanzibar inatakiwa kulipa kwa asilimia 168 badala ya asilimia 21  kwa uniti.

Shamhuna alikuwa akichangia katika majumuisho ya mjadala juu ripoti ya Kamati ya Mawasiliano na Ujenzi ya Baraza la Wawakilishi Zanzibar ambapo Shamuhuna  alisema, “hatukubali kulipa deni la shilingi bilioni 40 kwa kiwango cha asilimia 168 asiliani.”

Shirika la Tanesco ilipandisha viwango vya malipo kwa wateja wake tokea mwaka jana kwa asilimia 21, kwa upande wa Tanzania bara ambapo kwa Zanzibar shirika hilo la umeme ukapandishwa kwa asilimia 168 na kusababisha malalamiko makubwa upande wa Zanzibar.

Shamhuna alisema kuendelea kwa Tanesco kudai deni hilo kunakwenda kinyume na agizo la Rais Jakaya Kikwete kwamba pande zote mbili za Muungano zilipe viwango sawa vya asilimia 21 kulipa umeme na sio Zanzibar peke yao kupandishiwa bei jambo mbalo alisema sio sahihi.

Waziri huyo ambaye alikuwa akichangia na kupigiwa makofi na wajumbe wengine alisema ili kuepukana na utegemezi wa umeme kutoka Tanesco ambao unaigharimu SMZ fedha nyingi, serikali umeanza kuchukua hatua za kuzungumza na wawekezaji wazoefu ili kuzalisha umeme kutokana na jua na gesi utakaojitegemea.

Shamhuna aliwamabia wajumbe wa baraza la wawakilishi kwamba mradi kama huu umefanikiwa Dubai na Malaysia unaweza kuzalisha kati ya Megawati 50 na 100 ambao unatosheleza mahitaji ya sasa ya Zanzibar ya Megawati 50.

Hata hivyo, akizungumzia kuhusu madai ya baadhi ya Wajumbe wa baraza la Wawakilishi la kutaka Zanzibar izalishe umeme kwa kutumia mawimbi ya bahari, Shamhuna alisema utafiti unaonyesha kuwa ni mradi mkubwa wenye gharama kubwa na pia haujafanikiwa katika nchi nyingi duniani.

wakichangia mjadala huo wajumbe wengine wa baraza hilo wamesema suala hilo linahitaji kuangalia vyema na serikali ya muungano kwani haiwezekani serikali hiyo kukaa kimya na baadhi yao kutaka fedha hizo kutolipwa kwani haitowezekana kungangania fedha hizo.

Katika hatua nyengine wajumbe wa baraza la wawakilishi wamehoji juu ya majenereta 32 yaliyonunuliwa mwaka jana na kugharimu shilingi 17 billioni ili kukabiliana na tatizo la umeme Zanzibar kutotumika wakati huu ambao kuna matatizo ya umeme.

Wajumbe hao wamesema kuna taarifa kwamba majenereta hayo ni mabovu na wengine kutoa kauli za kutofanya kazi kutokana na kukosekana kwa mafuta maalumu ya kuendeshea majenereta hayo jambo ambalo lilihitaji majibu kutoka serikalini.

Shamuhuna aliwaambiwa wajumbe hao kwamba majereta yote 32 ni mazima, lakini yameshindwa kufanyakazi kutokana na ukosefu wa fedha za kununua mafuta za kuyaendesha jambo ambalo linahitaji kupatikana fedha za kutosha.

Baraza la wawakilishi limefungwa hapo jana hadi juni 15 ambapo kikao kitakachofuata kitakuwa ni cha kujadili bajeti, jumla ya maswali 88 kati ya 147, yaliulizwa na kujibiwa na miswaada minne ya sheria kupitishwa katika kikao hicho.

Advertisements

6 responses to “SMZ yagoma kuilipa TANESCO

  1. Nawashangaa sana Serikali ya ZNZ inashindwa kuzalisha megawati 50? Hivi kweli wataalamu wenu wanafanya nini? Anagalau huko bara kunahitajika Megawati zaidi ya 1000,na hata hivyo mikakati ingewekwa sawa bila mikingamo ya hao wanaojineemesha wenyewe tungeweza, fanyeni haraka achaneni na huo ukiritimba wa utegemezi tokea uhuru hadi leo mko wapi?

  2. Hapa inaonesha kuwepo umeme wa Tanesco Zanzibar sio kwaajili ya udugu na muungano uliopo, lakini kwaajili ya biashara ambayo itaipatia Bara faida maradufu. Kutokana na hayo, inaonesha wazi kuwa Tanesco inaichulia Zanzibar ni nchi ya kigeni kama zilivi nchi nyenginezo. Ama kuhusu petroli ya Zanzibar, upo udugu kwasababu ni petroli hiyo ni mali ya muungano.
    Quote

  3. In short, tanzania bara a.k.a tanganyika inaidhulumu sana zanzibar.inaiingizia hasara ambazo haziwahusu kabsaaa. maana uzembe wa serikali wa kuingia mikataba hovyo na dowans, ndo inayoumiza wenzetu wanzazibar hivi sasa kwa hiyo asilimia 168.yaani ufisadi wote unafanywa na wabara, kuanzia twin towers,ndege ya rais, rada, meremeta na mengine chungu nzima. yote haya yanaiumiza zanzibar kwa kiasi kikubwa mno. hivi lini tumeckia serikali ya zanzibar imefanya ufisadi?..yaani narudia tena serikali ya tanganyika inaiua serikali ya zanzibar kiuchumi kutokana na uzembe wa viongozi wetu wa bara

  4. NAMPONGEZA WAZIRI SHAMUHUNA KWA UJASIRI WA KUA MUWAZI KTK KIWANGO KILICHOTAKIWA KILIPWE NA TANESCO KUA NIKINYUME NA TARATIBU YA KAULI YA RAIS JK,ZANZIBAR IMEFIKA WAKATI SASA KUFIKIRIA NJIA MBADALA YA KUZALISHA UMEME WAKE WENYEWE NA HILO LINAWEZEKANA ZIKO NCHI NYINGI DUNIANI NA NI VISIWA KAMA SISI NA WANAJITEGEMEA KWANINI ZANZIBAR ISHINDIKANE UMEFIKA WAKATI TUAMUE JUU YA UZALISHWAJI UMMEME ZANZIBAR

  5. dalili zinanonesha tanesco inatumiwa kama hakiba ya chambo cha mbeleni. 21% na 168% ni tafauti ya mbingu na ardhi….
    kama mazungumzo ya kikatiba na muungano hayakufikia makubaliano inawezekana madeni ya tanesco yaliyokuwa inflated yakatumika kutu-arm twist wazanzibari tukubali conditions zao…hakuna jengine linaloingia akilini hapa, kwa hivyo tutahadhar sana na hilo.

  6. NYINYI VIONGOZI HAMUJASIKIYA KAMA KUNA KITU KINAITWA WINDAPOWER AMBACHO KINAZALISHA UMEME KILA SIKU MUNASAFIRI MUNAKWENDA NCHI ZA NJE MUNAFANYA NINI SS?? HAINA HAJA YA KUWATEGEMEYA WATU WA TANGANYIKA MUNAWEZA KUNUNUWA WINDPOWER MAGUZO MATATU UNGUJA NA MATATU PEMBA KWISHA WATU WOTE WATAKUWA NA UMEME NA MWENGINE MUTATAFUTA PAKUWEKA MUWE HAMUNA KWA JINSI ULIVYOKUWA NA NGUVU MUNAKA MUKIBABAISHWA NA WATU WA TANGANYIAKA MARA KUNDE MARA MBAAZI NINI NYINYI VIONGOZI HEBU SIMAMENI NA MIGUU YENU WACHENI KUWATENGEMEYA BARA KILA KITU MUONE KAMA HATUTOSOGA MBELE HARAKA KULIKO KUSHIRIKIANA NA WAO NA MATHILA NA MAUTH YA ROHO TU NDIO TUNAYOYAPATA.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s