serikali yatakiwa kuwa makini

Mwakilishi wa Mji Mkongwe wa Chama Cha Wananchi (CUF) Ismail Jussa Ladhu akizungumza katika kikao cha Bunge wakati akiwa mbunge mteule wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete katika bunge lililopita kabla ya uchaguzi mkuu kufanyika mwaka jana

MATUMIZI mabaya na upotevu wa fedha za serikali bado yanaendelea kuitesa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar baada ya kamati ya Mahesabu ya Serikali (PAC) kubainisha kuwapo upotevu mabilioni shilingi ya fedha za serikali katika kikao cha baraza la wawakilishi.Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi kabla ya kufungwa kikao chao walilamikia hatua ya fedha za serikali zinavyopotea wakati wakitoa maoni yao katika kamati ya kuchunguza mahesabu ya serikali PAC, kikao kilichomalizika juzi katika ukumbi wa Baraza la Wawakilishi Mbweni nje kidogo ya Mji wa Zanzibar.


Wawakilishi hao waliitwisha serikali lawama hizo na kuwalaumu Makatibu Wakuu na Wakurugenzi katika Mawizara kushindwa kuwajibika vyema katika fedha za serikali ambapo walisema kuwa inashangaza kuona matukio ya upotevu wa fedha za serikali umekuwa ni wa kujirejea mwaka hadi mwaka huku kukiwa na sababu zisizofutika katika miaka yote.
Hali hiyo wajumbe hao waliieleza kinachoonekana kwa watendaji hao kuthubutu kufanya hivyo kutokana na sheria ya sheria namba 9, ya mwaka 2005 ya manunuzi na kuziondoa mali za umma haiwapeleki mahakamani wahuska wake jambo ambalo serikali itapaswa kuona sasa hilo linafanyika kwa ripoti zitazooenesha kuwapo kwa hilo.

Walisema wanashangaa kuona Zanzibar imekuwa inashindwa kuchukua hatua za kuwafikisha watendaji wasiowajika vizuri kwa matumizi ya fedha za serikali wakati upande wa Tanzania bara ikiwa wanafikishwa mahakamani.Walisema kuanzia sasa ni vyema kwa serikali kuona inawafikisha mahakamani wahusika wote huku ikiwawajibisha hadi makatibu Wakuu katika Mawizara za serikali.
Mwakilishi wa Mji Mkongwe (CUF) Ismail Jussa Ladhu, alisema, haja ya kuchunguzwa kwa hoteli ya Bwawani mikataba yake bado serikali inapaswa kuiangalia kwani mkataba wa ukodishwaji ukumbi wa disko unaonekana haukuwa katika hali ya kufuata misingi ya kisheria na hoja ya kuwa aliyekodishwa ana uzoefu haina msingi.
Jussa alisema muwekezaji aliyepewa wa marketing International amekodishwa kwa shilingi 15,000,000 lakini amelipa shilingi 10,000,000 na shilingi 5,000, 000 hajatoa kwa vile amedai ni fedha za matengenezo ukumbi huo wakati suala hilo halimo ndani ya makubaliano ya mkataba wake.
Mwakilishi huyo kijana alisema serikali kutokana na hali hiyo imekuwa ikipata hasara kubwa kutokana na kuacha kuchukua mkataba wa shilingi 35,000,000 wa Star na Zenj FM shilingi 24,000,000 na kupewa wa 15,000,000 ambaye analipa shilingi 10,000,000 badala ya milioni 15 walizokubaliana.
Akiendelea kuchangia hoja hiyo Jussa amesema tatizo la ukodishaji pia imekikumba kisiwa cha Changuu ambapo sasa kimekodishwa kwa dola za kimarekani 8,000 lakini jambo la kushangaza muwekezaji aliepewa kisiwa hicho hivi sasa anatoa dola za kimarekani 3,000 tu hivyo serikali ilitakiwa kutazama kwa umakini katika suala hilo ambalo serikali hukosa mapato makubwa kutokana na kutozingatiwa mikataba inayofungwa kati ya serikali na wawekezaji.

Aidha Jussa aligusia suala zima la upotevu wa fedha za serikali katika Afisi ya Biashara, Viwanda na masoko ambapo gari alilokuwa afisa mdhanini liliuzwa baada kuonekana limechakaa lakini cha kushangaza gari hilo lilo limeuziwa tena serikali huku akiwachekesha wawakilishi kwamba serikali iwe makini katika masuala la fedha za serikkali isije kuangukia kama ilivyofanyika miaka ya nyuma ambapo gari la rais lilizimika moto njiani kutokana na tabia ya watendaji kufanya vitendo kama hivyo.
Mwakilishi huyo wa Mji Mkongwe alisema serikali anakubaliana na kudai deni lake katika shirika la Ndege Tanzania ATC kwani haiwezekani TANESCO ikawa inadai madeni yake ya matumizi ya umeme lakini serikali ikae kimya katika madeni yake kwneye taasisi za muungano.
Mwakilishi wa Kitope, Makame Mshimba, akichangia hilo alisema umefikia wakati wa kuona serikali inawafikisha mahakamani wahusika wote waliobainika kupoteza fedha za serikali kwani wanaimani kuwa hazipotei bali baadhi ya watu wamekuwa wakinufaika nazo.Kwa upande wake Mwakilishi wa Jimbo la Kwamtipura Hamza Hassan Juma, alisema serikali iliangalie suala la ununuzi wa majenereta mapya ya ZECO baada ya kuwapo kwa taarifa ya majenreta saba tayari yanashindwa kufanya kazi kutokana na kuharibika.
Alisema ni vyema kwa serikali kuyaangalia hayo kutokana na hivi sasa nyingi ya mali za serikali zinaonekana kufanywa sawa na mashamba ya bibi huku akitishai kuzuiya bajeti ya Wizara ya fedha baada ya kuitaka shirika la ZSTC kusamehe deni lake la shilingi biloni 4/= na kulipa bilioni 1/= ambapo alisema hali hiyo itauwa Shirika hilo.
Akiwasilisha ripoti yake Mwenyekiti wa kamati ya PAC, Omar Ali Shehe alisema Ripoti ya Mdhibiti Mkuu wa serikali ya mwaka 2005/2006 fedha zilizopotea ni 1,721,401,530.35 huku fedha za kigeni zikiwa ni dola za kimarekani 378,844.92.
Lakini katika ripoti ya mwaka 2006/2007, alisema Mwenyekiti huyo fedha zilizopotea ni 1,273,364,649 huku fedha za kigeni zikiwa ni dola za kimarekani 72,893 na mwaka 2007/2008 zilizopotea ni shilingi 269,757,772 na fedha za kigeni zikiwa ni dola za kimarekani ni 145,480.Mwenyekiti huyo alisema upotevu zaidi wa mali za serikali umekuwa ukijionesha katika ukosefu wa vielezo wa mali za serikali huku kukiwa na baadhi ya watendaji kupandishia gharama kwa wanunuzi wa vifaa vya serikali huku wengine wakitumia mwanya walionao katika kusimamia kazi za ujenzi.
Shehe alisema mmoja wa fundi ujenzi aliiambia kamati hiyo hiyo kuwa alipewa kazi na moja ya taasisi ya serikali na kutaka kulipwa gharama ya shilingi 2,000,000 lakini alipopewa vocha kusaini iliyokuwa na shilingi 20,000,000 ambapo aligoma lakini baada ya majadiliano marefu alipewa shilingi 500,000 ili akubali kusaini ambapo kamati hiyo imepatwa na wasi wasi na gharama zinazotumika kwa shughuli za ujenzi na miradi ya maendeleo.

Wakijibu hoja za Wajumbe hao Mawaziri wa Serikali akiwemo waziri wa Fedha, Uchumi, Mipango ya Maendeleo, Omar Yussuf Mzee alisema serikali imeshatowa agizo kwa watendaji wote wa serikali kuorodhesha mali za serikali.Alisema agizo hilo mwisho wa kulitekeleza ni mwezi Juni ambapo serikali baadae itakaa na kuangalia namna ya kufanya katika kufanya tathmini halisi.Waziri huyo alisema mengi ya mashirika ya serikali hivi sasa yanaonekana kutofanya vizuri na hivi sasa serikali inajiandaa kuyafuta baada ya kubaini baadhi ya mashirika hayo kuwa na wafanyakazi wengi, huku yakiwa hayana mtaji na yanashindwa kuleta tija kwa serikali.

Alisema haiwezekani kuendelea kuwa na mshirika ambayo hayana tija kwa serikali kutokana na hivi sasa imekuwa ikitumia zaidi ya shilingi bilioni 7/= kwa ajili ya ruzuku.Waziri wa afisi ya Rais Ikulu, Dk. Mwinyihaji Makame, alielea kuwa katika kudhibiti matatizo upotevu wa fedha za serikali hivi sasa tayari serikali inakamilisha mabadiliko ya uundwaji wa serikali za mitaa.
Waziri wa Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Haji Omar Kheir, alisema serikali itahakikisha ripoti za mdhibiti na mkaguzi wa serikali inazifanyia kazi kwa kuwawajibisha wahusika wake baada ya kuwaita na kuelezwa uovu wao.Waziri wa Katiba na Sheria Abubaka Khamis Bakari, alisema kuanzia sasa serikali inapaswa kufikiria kuwapandisha Mahakamani wahusika kwani inaonekana vitendo hivyo vikiacvhiwa huenda vikaendelea.
Waziri wa Miundombinu na Mawasiliano alisema ni kweli SMZ inalidai ATC 200 miloni deni ambalo la mwaka 2008 na hivi sasa tayari wameanza kulishughulikia suala hilo katika vikao vya Muungano na matokeo yake yanaonekana huenda yakawa mazuri.Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali, Ramadhan Abdalla Shaaban, alisema Wizara yake itashirikiana na serikali kuona ripoti za kamati hiyo inazifanyia kazi.Waziri wa Afya, Juma Duni Haji, alisema wafanyakazi sita ambao serikali iliwazuiliya mishahara yao kutokana na tuhuma za ubadhirifu wa mishahara hewa, ambapo tayari imeshawalipa mishahara watumishi wanne na wawili wizara hiyo inatarajia kuwalipa mwezi huu.
Waziri wa Wizara ya Uwezeshaji, Maendeleo ya Vijana Wanawake na Watoto Zaina Omar Mohammed, alisema atashirikiana na serikali kuona wanaimarisha utawala bora katika kutumia fedha za serikali.Nae Waziri wa habari Utamaduni Utalii na Michezo, Abdilah Jihad, alisema kuwa wizara yake itahakikisha inaiangalia upya mikata yake ikiwa ni hatua itayowezesha kufuata taratibu za kisheria.

Nae Waziri wa Ardhi, Makaazi, Maji na Nishati, Ali Juma Shamhuna, alisema hakuna ukweli juu ya taarifa za kuharibika kwa majenreta mapya bali yanashindwa kuwashwa hivi sasa kukabiliana na tatizo la mgao kutokana na hakuna mafuta ya kuendeshea majenereta hayo.Waziri wa Biashara, Viwanda na Masoko Nassor Mazrui, ameeleza kuwa Wizara yake itaendelea kusimamia majukumu yake ikiwa pamojana suala la wafanyabishara kutozwa kodi mara mbili.
Akifunga mjadala huo Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Omar Shehe ameliomba Baraza la wawakilishi kumuomba Rais wa Zanzibar kutoa neno zito juu ya ripoti ya mkaguzi wa serikali kwa watendaji wa serikali ikiwa hatua ambayo inaweza kusaidia kuondokana na vitendo hivyo kwani alieleza Zanzibar inaweza kuimarika bila ya usifadi.

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s