Fedha za serikali zisivujishwe

Makamu wa Pili wa Rais Balozi Seif Ali Iddi akifunga kikao cha baraza la wawakilishi kilichokitimishwa hapo jana siku ambapo pamoja na mambo mengine amezungumzia suala la uwajibikaji kwa viongozi wa serikali

MAKAMU wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Idd amewaagiza viongozi wenye dhamana ya kusimamia fedha kuwajibika ipasavyo kwa kusimamia majukumu yao kiamilifu ili fedha za serikali zisipotee ovyo.

Akifunga kikao cha baraza la wawakilishi kilichodumu kwa wiki mbili hapa Zanzibar Balozi Seif alisema ripoti ya mdhibiti na mkaguzi wa hesabu za serikali ya mwaka 2008/2009 imeonesha kuwepo ukiukwaji wa taratibu na udhibiti wa fedha na mali za serikali kwa baadhi ya taasisi za umma.

“Natoa agizo kwa makatibu wakuu, wakurugenzi na wale wote wanaosimamia fedha za serikali wawajibike ipasavyo kwa kusimamia kwa ukamilifu mapato na matumizi ya fedha za serikali” alisema Balozi Seif.

Alisema jambo hilo litakwenda sambamba na sheria namba 9 ya mwaka 2005 ya manunuzi na kuziondoa mali za umma pamoja na kanuni za fedha zilizopo.

Aidha alisema ni wajibu wa mamlaka zote husika na usimamizi wa mapato kupanua wigo utakaosaidia uendeshaji mzuri wa serikali na kutoa huduma za maendeleo ya jamii katika nchini.

“Ni wajibu wa mamlaka zote zinazohusika na usimamizi wa mapato, kupanua wigo utakaosaidia uendeshaji mzuri wa serikali na kutoa huduma za maendeleo ya jamii,” alisema.

Wakati huo huo Balozi Seif amewaagiza wakuu wa mikoa na wilaya kujiepusha na vitendo vinavyochangia kuibuka kwa migogoro ya ardhi Zanzibar .

Alisema iwapo viongozi hao watakuwa sehemu ya watu wanaovamia ardhi, watashindwa kushughulikia kero za migogoro midogo midogo ya ardhi inayowakabili wananchi.

Kiongozi huyo alisema uvamizi wa ardhi kwa ajili ya ujenzi wa nyumba za makazi, biashara na uwekezaji katika kilimo umenazidi kuongezeka kuzua malalamiko katika jamii katija sehemu nyingi mijini na vijijini Unguja na Pemba .

Alisema wakati serikali inajipanga kukabiliana na tatizo hilo , basi wakuu wa mikoa na wilaya wakae mbali, ili kuepuka kuwa sehemu ya chanzo cha migogoro hiyo katika maeneo yao .

“Suala la uvamizi wa ardhi halikubaliki kwa mujibu wa sheria na taratibu tulizojiwekea,” alisema Balozi Seif na kuwataka viongozi hao kuwa mstari wa mbele katika juhudi ya kushughulikia migogoro hiyo katika maeneo yao  

Alisema migogoro ya ardhi ikiachwa kuendelea bila kupatiwa ufumbuzi, taifa linaweza kupoteza amani, umoja na mshikamano kutokana na wananchi kukata tamaa kuhusu hatma ya maisha yao ambapo kwa sasa wananchi wengi wamekata tamaa katika maisha yao kutokana na vitendo hivyo.

Akizungumzia suala la hatma ya Zanzibar kujiunga na jumuiya ya kiislamu ya OIC, Balozi Seif alisema tangu mwaka jana sekretarieti ya OIC ilivunjwa na kuundwa kamati mpya ambayo itaangalia upya muundo wa taasisi hiyo na masharti kwa wanachama wapya.

Alisema wakati inatekeleza zoezi hilo , OIC ilisitisha kupokea wanachama wapya na kwamba baada ya zoezi hilo kikamilika mwakani, Tanzania itatafakari tena juu ya uwanachama katika taasisi hiyo.

Balozi Seif alimalizia kuwaeleza wajumbe kwamba licha ya changamoto zilizopo zinazoikabili Zanzibar katika kuiletea maelendeo “imani yenu na ushirikiano wenu mnaoendelea kutoa kwa serikali, unatupa moyo na za matumaini kwamba kwa pamoja tutaweza kukuza uchumi, kuongeza ufanisi katika utoaji huduma za jamii na hatime kupunguza umasikini kwa wananchi, na kuleta maisha bora kwa wote” alisema Balozi Seif.

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s