Mtaishia upolisi tu

Waziri anasema wazanzibari hawana sifa na vigezo vya kuingia jeshini kutokana na kutokuwa na vyeti hilo ni kweli lakini au kuna sababu nyengine zaidi ya hiyo?kufuatia hilo ndio vijana kutoka Tanzania Bara wanakuja Zanzibar kuja kuwania nafasi hizo na matokeo yake huingia jeshini kupitia fursa hiyo si wazanzibari hawana vyeti basi wao wanakuja navyo na wanaomba wakiwa hapa hapa

Tatizo vijana wetu hawana sifa SMZ

SERIKALI ya Mapinduzi ya Zanzibar imetoa maelezo juu ya vijana kutoka visiwani kukosa ajira katika Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kuwa inatokana na kukosekana sifa za kujiunga na jeshi hilo.

Waziri wa Nchi katika Ofisi ya Rais, Mwinyihaji Makame Mwadini, alisema jana kuwa vijana wengi kutoka visiwani wanashindwa kupata ajira katika jeshi hilo kwa kukosa sifa na viwango vyao vya elimu kuwa vidogo.

Mwadini alikuwa anajibu swali la nyongeza la Mahmoud Muhammed Mussa (Kikwajuni) juu ya vijana wa Zanzibar waliopitia mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) kutoajiriwa na JWTZ.

Mussa alisema jeshi hilo mwaka jana liliajiri zaidi ya vijana 200, lakini kati ya hao hapakuwepo wa kutoka Zanzibar.

Akifafanua Waziri Mwadini alisema, ingawa vijana waliomaliza elimu ya sekondari wanapewa nafasi kubwa na JWTZ katika ajira ya jeshi hilo, vijana wengi kutoka Zanzibar wanakosa fursa hiyo kwa kukosa sifa, ikiwa ni pamoja na kutokuwa na vyeti.

“Vijana wetu wengi hawana vyeti, na kama wanavyo ni vya kufoji na pia wanafeli interview,…ajira jeshini siku hizi inazingatia suala la elimu,” alisema.

Mwadini alisema vijana kutoka Zanzibar wanapoitwa kwenda kufanya usaili jeshini wanashindwa kusema hata sentensi moja kwa Kiingereza.

Akijibu swali lingine la nyongeza la Makame Mshimba Mbarouk kwamba kutowaajiri vijana kutaongeza ujambazi, Mwadini alisema vijana wajengewe msingi wa kufanyakazi za kujiajiri.

Alisema chini ya sheria ya mwaka 2003, Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inatoa fursa kwa vijana kupata emafunzo kupitia Jeshi la Kujenga Uchumi (JKU) nia ikiwa ni kuwawezesha kujiajiri.

Alisema chini ya utaratibu huo mafunzo hayo yanatilia mkazo elimu ya taalima za nyanja mbali mbali, zikiwemo za kilimo, uvuvi na ufundi.

Hatutawachukulia hatua zozote

SERIKALI haina mpango wa kuwachukulia hatua za kisheria watu wanaorejea katika akili ya baada ya kutibiwa ugonjwa waliopata kwa kutumia madawa ya kulevya.

Waziri wa Fedha, Uchumi na Mipango wa Zanzibar , Omar Yusuf Mzee alisema jana kuwa ni kinyume cha sheria kumfikisha mahakamani aliyepona ugonjwa, hata kama aliupata kwa njia ya uhalifu.

“Si jambo jema kumwadhibu mgonjwa anapopata hujambo, baada ya kutibiwa kwa gharama za serikali,” alisema Mzee.

Alisema kugharamia matibabu ya wagonjwa mbali mbali, wakiwemo wanaosumbuliwa na maradhi ya akili ni miongoni mwa majukumu ya serikali kwa wananchi.

Waziri Mzee alikuwa anajibu swali la nyongeza la Fatma Mbarouk Said (Amani) aliyesema wapo wagonjwa wa akili wanaopata ugonjwa huo kwa kutumia madawa ya kulevya na kutaka kujua hatua zinazochukuliwa dhidi yao baada ya kutibiwa kwa gharama ya serikali na kurejea katika akili ya kawaida.

Akijibu swali la msingi la Jaku Hashim Ayub (Muyuni) juu ya kutotekelezwa kwa mradi wa afya ya akili licha ya serikali kutenga sh. milioni 95 mwaka jana na fedha hizo kutopelekwa wizara ya afya.

Mzee alisema baraza liliidhinisha jumla y ash. Milioni 107 lakini hazikutolewa kwa sababu hazikupatikana kwa sababu fedha hizo zilipaswa kutokana na ufadhi wa wahisani.

WAJUMBE wa Baraza la Wawakilishi, wamependekeza iundwe tume ya kuchunguza kuwepo kwa mikataba yenye utata katika Manispaa ya Zanzibar .

Wajumbe hao walitoa pendekezo hilo jana wakati wanajadili ripoti ya kamati ya baraza hilo ya kusimamia ofisi za viongozi wakuu wa kitaifa, juu ya utekelezaji wa kazi za kawaida na za maendeleo.

Ripoti hiyo ilisomwa katika kikao cha baraza hilo kinacoendelea mjini hapa na Makamu Mwenyekiti wa kamati hiyo, Mwanajuma Faki Mdachi.

Akijadili ripoti hiyo Makame Mshimba Mbarouk (Kitope) alisema, “kuna wimbi kubwa la mikataba ya ubabaishaji, kiasi kwamba manispaa inaweza kushtakiwa.”

Alisema April 23, mwaka 2006 Manispaa ya Zanzibar iliingia mkataba wenye thamani ya Sh. milioni 700 na Kampuni ya simu za mkononi Zantel, lakini imeshindwa kuuheshimu mkataba huo.

Chini ya mkataba huo, Zantel ilipewa nafasi ya kuweka mabango, yaani Billboards za kuuza biashara yake katika manispaa hiyo, lakini kila yanapowekwa mabango hayo yanashushwa badala yake yanaonekana ya kampuni nyingine, pia ya simu za mkononi.

Zantel ina mkataba uliofikiwa kisheria, lakini kila inapoweka mabango yake, viongozi wanaagiza yatolewe, alisema Mbarouk na kuongeza “iundwe tume hapa kuna mchezo mchafu.”

Mbarouk alisema kuwepo kwa ubabaishaji katika mkataba huo ni dalili ya rushwa miongoni mwa watendaji wa Manispaa ya Zanzibar na wengine serikalini.

Alisema anapendekeza iundwe tume kwa sababu kuonekana kwa mabango ya kuuza biashara ya kampuni nyingine tofauti Zantel ni dalili kwamba kampuni hiyo imeruhusiwa kuweka mabango hayo kinyemela.

Hoja ya Mbarouk juu ya kuundwa tume ya baraza pia ilungwa mkono na wajumbe watatu wa baraza hilo , Abdalla Juma Abdall (Chonga), Salmin Awadh Salmin (Magomeni) Hija Hassan Hija (Ziwani).

Hija kwa upande wake alisema taarifa kwamba wajumbe wa kamati walidharauliwa wakati wanachukunguza utendaji wa Manispaa ya Zanzibar .

Juu ya tatizo la umeme katika ukumbi wa Baraza la Wawakilishi, Awadh alisema ukosefu wa jenereta limezungumzwa kwa kurudia rudia lakini mpaka sasa halijapatiwa ufumbuzi.

Alisema unapokosekana umeme wa kawaida, shughuli za baraza zinasitishwa na kusababisha serikali kupata hasara kwa kuongeza muda wa vikao.

“Ni jambo la aibu jengo hili kukosa jenereta,” alisema na kwamba mbali na ukosefu wa jenereta, jengo hilo pia muundo wa jengo jipya la baraza na vifaa vinasababisha sauti kutosikika vizuri.

“Sauti hazisikiki vizuri ndani ya ukumbi wa baraza na kusababisha wazungumzaji kuomba kurudia rudia kila wanachozungumza,….tunatumia muda mwingi na nguvu kuwasikiliza wazungumzaji,” alisema Awadh.

Pamoja na maeneo mengine, ripoti iliyowakilishwa na kamati katika kikao cha baraza hilo juu ya utekelezaji wa kazi za kawaida na za maendeleo, zinazosimamiwa na ofisi za viongozi wakuu wa kitaifa, imegusa Ofisi ya Rais, Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais na Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar.

Wakati huo huo, Spika wa Baraza la Wawakilishi, Pandu Ameir Kificho, alisema jana kikao cha baraza hilo kitaendelea kama kawaida leo kufidia muda uliopotea kwa kuahirisha shughuli za baraza mara kwa mara umeme unapokosekana ukumbini.

Advertisements

12 responses to “Mtaishia upolisi tu

 1. Hivi huyu bwana mwinyihaji anaakili kweli ? yaani vijana wa zanzibar kutokuwa na vyeti alaumiwe nani na nani kamwambia jeshini kunaenda wasomi na polisi ni mambumbumbu? na atwambie pia sirekali yake imejipanga vipi kuhakikisha watoto wa kizanzibari wanaelimika ipasavyo ili nawao pia wafaidike na kazi za jeshini? mimi siamini kwamba vijana wa znz hawana vyeti bali ni huo ni msukumo wa watanyanyika kutaka wazanzibar wasiende jeshini .

  • ebwana mm nasema ni uongo kwa kiasi hasa coz kila mwaka zanzibar inatoa wanafunzi je katumia takuwimu gani mpaka anasema haya halafu tunamuomba aainishe na vigezo vinginevyo ili uweze kuingia jeshi? lkn hawa ndio viongozi we2 hahitajika marekebisho hasa

 2. Naomba nitowe historia yangu.
  Baada ya kumaliza advance level hapa Zanzibar niliingia JKU. Baada ya miezi 2 tuliitwa kwenye mkutano na Mkuu wa JKU. Tulikuwa vijana 18 waliomaliza form vi katika mkumbo ule. Tulipofika hadithi ilikuwa hiyo kuwa tuntakiwa tujiunge na jeshi, kwani hakuna wasomi. Alitwambia mara tukifika tutaanza na afisa cadet (nilikuwa sijuwi ninini). Tulimuomba atupe muda tujishauri, akakubali.

  Wengi tuliogopa, lakini baada ya kushawishiana ilipofika siku sote tulisema tuko tayari. Akatuahidi watakuja kuchukuwa vipimo na kufanya usajili. Amma mpaka nimekimbia hakuna aliyekuja. Baada ya miezi 6 kupita walikuja baadhi ya rafiki zangu walikuwepo. Walichofanya walichukuwa vijana watatu wenye asili ya Bara, wale wengine wote wenye asili ya Kizanzibar kutoka Kiboje, Chaani, Nungwi,nk hakuna aliyechukuliwa.

 3. Ndio tuamini kwamba tunatawaliwa kwa nguvu iweje tuna wizara ya elimu na mitihani itoke bara jee tunategemea vipi kufaulu wakati kila kitu katika kiwango znz na tanganyika ni tofauti ? jambo la muhimu hapa ni kuvunja tu muungano wenyewe.

 4. ss ww waziri unawalaumu vijana wa taifa lako kuwa hawana vyeti ss ww waziri kazi yako nini kama sio kuwasaidiya wakawa na vyeti pili musitudanganye kabisa kuwa hao majeshi na polisi wa bara waliyoja znz wote wanajuwa kiengereza hawajuwi hata kusema good morning munatuambiya wazanzibar hawjuwi kiengereza ndio maana hawachukuliwi jeshini na polisi jeshi kubwa duniani ss ni wamarekani je hilo jeshi lao munawajuwa hao wanajeshi wao ni nani???kama hamujuwi mm nitawambiya ni walatino kutoka southamerika ambao wamawambiya wajiunge na jeshi wapinganiye amerika ndio watawapa paspoti za amerika na familiya zao na vijana wengine ni watu waliyofeli mitihani ya kwenda chuo kiku na wengine ni maghetto boys abao hawajawahi kwenda skuli ndio majeshi wa marekani na ndio tishio ulimwengu mzima leo munatuambiya ati znz hawakusoma ndi hawawezi kuwa jeshi kwani kuilinda nchi yako unatakiwa ujuwe kiengereza mbona wamerekani na west europ hawawambi majeshi yao lazima mujuwe kirussi na kichina na kiswahili ndio muwe majishi wacheni kuwadanganya watu nyenye ni wamaziri na majeshi ya bara yanawalinda nyinyi na kuwakandamiza wazanzibar munajuwa kama wangelikuwa majeshi ni wazanzibar na munawakandamiza dada zao na mama zao na baba zao na jamaa zao wengeliwapinduliya mbalini ndio maana hii ni 2011 watu washamka tutavunja muungano feki kisha na nyinyi pia mutajiuzulu kwa lazima na pia mutatueleza mali mulizo nazo mumezipata vipi huwezi kujibu tutazisha koti hapo hapo znz yakuwahukumu nyinyi viongozi wabaya muliyo iyuza znz kwa faida ya matumbo yenu na hiyo ni hapa duniani tu bado kesho akhera ALLAH anawasubiri akawaweke sawa kabisa .

 5. Tatizo sio vyeti wala intervew, ukweli nikwamba serikali wizara ya ulinzi na jeshi la kujenga taifa (jkt) walaumiwe kwas

 6. Tunaiomba serikali iwapatie ajila vijana wanaopitia jkt, ili kuondoa lawama na vitisho wanavyo towa vijana wanapokosa aj

 7. Operetion kilimo kwanza, tunaishangaa serikali, wizara ya ulinzi, na jkt.! tumelijenga sana Taifa, kwanini tusiajiliwe??

 8. wamozoea si mara ya kwanza ,kuna muakilishi mmoja tena mwanamke kathubutu kusema kuwa waz’bar wavibu w kufanya kazi, jambo la kustajabisha leo munatuambia kwamba mutachukua hatua kali kwa wale wanaokwenda kusoma nje halafu wasirejee kufanya kazi nyumbani, iweje leo wakawa sio wavivu tena, nendeni kawachukueni hao hao watanganyika wenu waliokuwa mahodari wa kufanya kazi ya kujenga makanisa nchi nzima na biashara ya kuuza na na kuweka mabar hongereni wajumbe wa baraza la wawakilishi kwa ututukana 2mekupeni wenyewe haki yenu ss kutufanyia mnavyotaka akiomba mz’bar kazi hakuna lakini akija mtanganyika kazi atapewa tumeona tunawajua , munawaacha ndugu zenu wanazurura mitaaani au kuuza nguo darajani dada njoo

 9. kwanini vijana wanaopitia jkt wanazulula mtaani bila kazi, wakati serikali inaelewa kwamba vijana hao hawana ajira nawamepitia mbinu za kijeshi, inasikitisha sana, watanzania wenzangu, mimi ni miongoni mwa vijana wa jkt lakini nasikitika sana kuona mpaka sasa tunatabika kitaani, ubaguzi katika selikali yetu ni mkubwa sana, mbona vijana wanao tokea zanzibar wanaajiriwa kwanini sisi wa kutoka bara hatuajiliwi, sina amani na serikali ya muungano wa tanzania,

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s