Mazingira ni urithi wa watoto wetu

Bi Asha mke wa Balozi Seif Ali Iddi akizungumza na wananchi mbali mbali juu ya uhifadhi wa mazingira katika mkoa wa kaskazini Unguja

Wazazi wameshauriwa kuelimishana juu ya suala la utunzaji wa mazingira ili jamii ifaidike na maisha bora na kuwaachia watoto wao urithi wa mazingira bora ya kuishi.

Ushauri huo umetolewa na Mke wa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mama Asha Seif Iddi alipokuwa akizundua rasmi maadhimisho ya Juma la wiki ya Wazazi katika Mkoa wa Kaskazini Unguja yaliofanyika Bumbwini Makoba Wilaya Kaskazini B.

Mama Asha alieleza kusikitishwa kwake na vitendo vya baadhi ya watu wanaoiteketeza miti kwa kutumia misumeno ya moto bila ya kuzingatia athari za uharibifu wa mazingira.

Alisema ukataji wa miti ovyo usiozingatia utunzaji wa mazingira unaathiri nchi kwa njia nyingi ikiwemo kuwakosesha matunda ya kutosha wananchi na kukausha vyanzo vya maji ardhini.

Kwahivyo aliwataka wazazi kusimamia suala la mazingira katika maeneo yao na pia kuwaelimisha watoto wao kazi za amali ili waweze kujitegemea kwa kujiajri kwa kazi za amali na kuachana na ukataji miti ovyo kama moja wapo ya ajira zao.

Mapema mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Mkoa wa Kaskazni Unguja Mhe Mussa Ame Silima, alisema wameamua kupanda miti katika wiki ya maadhimisho ya juma la Wazazi kwa lengo la kukumbushana moja ya majukumu yao ya kushajiisha utunzani wa mazingira.

Uzinduzi huo wa Juma la Wiki ya Wazazi ulitanguliwa na zoezi la upandaji miti lililowajumuisha Mgeni rasmi na viongozi wengine waliohudhuria Sherehe hiyo.

Katika hatua nyengine imeelezwa kuwa muundo wa Serikali mpya ya Umoja wa Kitaifa wa Zanzibar ni tofauti na miundo miyengine ya Serikali za nchi nyengine Katika Bara la Afrika.

Hayo yalielezwa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe Balozi Seif Ali Iddi alipokuwa na mazungumzo na Balozi wa Canada nchini Tanzania Mhe Robert J. Orr yaliofanyika kwenye Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais iliyoko katika Baraza la Wawakilishi Mweni.

Mheshimiwa Balozi Seif Iddi alisema moja ya tofauti ni kuwa Serikali za Umoja wa Kitaifa za nchi nyengine ziliundwa baada ya uchaguzi kwa kuepusha migogano, wakati Serikali ya Zanzibar ilianzishwa ndani ya Katiba kabla ya Uchaguzi.

Kwahivyo alisema hata muundo wake haukuwa na matatizo katika uteuzi wa viongozi na ulifnywa kwa mashirikiano makubwa baina ya viongozi wakuu wa pande zote mbili za vyama huska.

Naye Balozi wa Canada Mhe Robert J. Orr alisema nchi yake nayo imo katika matayarisho ya uchaguzi unaotarajiwa kufanyka katika Mwezi wa Mei na kueleza matarajio yake kuwa wataendelea kutoa ushirikiano wao kama kawaida.

Aidha, alieleza haja ya kutoa vipa umbele katika kusaidia miradi ya maendeleo kama Sekta binafsi, kilimo na hata kushajiisha wawekezaji kuwekeza hapa nchini.

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s