Wawakilishi waoga waonekana

Mwenyekiti wa Baraza la Wawakilishi Mahmoud Mohammed Mussa ambaye pia ni Mwakilishi wa Jimbo la Kikwajuni kupitia tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) alikuwa akiendesha kikao cha baraza hilo leo alikuwa na wakati mgumu kidogo baada ya kuendesha kikao ambacho kilikuwa moto baada ya pande mbili kuvutana upande upande wa serikali na upande wa wawakilishi.

Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi leo waliingia katika mjadala mkali na wa kuvutana kati ya pande mbili moja upande wa serikali na upande wa pili ni wawakilishi kutoka pande zote mbili (backbenchers) kuhusu hoja ya kutaka iundwe Kamati Teule kuchunguza ufisadi kwenye Baraza la Manispaa la Zanzibar.

Hoja ilikuwa kuchunguza tuhuma za ubadhifu mkubwa na rushwa katika Manispaa huku Waziri na baadhi ya maafisa wakitajwa kuchukua 10% lakini Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Dk Mwinyihaji Makame Mwadini alipinga vikali kuhusika na tuhuma hizo na kumtaka Mwakilishi Makame Mshimba Mbarouk wa Jimbo la Kitope (CCM) aliyetoa tuhuma hizo aombe radhi ndani ya baraza hilo lakini Mwakilishi huyo alikataa kuomba radhi kabisa na kushikilia msimamo wake kwamba ikiwa tuhuma sio za kwlei basi kamati teule ndio itasafisha tuhuma hizo na sio kuombwa radhi Waziri.

Hatimae baraza la wawakilishi chini ya Mwenyekiti wake Mahamoud Mohammed Mussa akaamua kupigwe kura ya kuulizwa kama wajumbe wanakubaliana na kuundwa kamati teule bau laa walipoulizwa wajumbe jumla ya wajumbe 29 walitaka uindwe kamati teule na wajumbe 28 walikataa isiundwe.

Lakini baadae alisimama Waziri wa Katiba na Sheria, Abubakar Khamis Bakari na Mwakilishi wa Jimbo la Mgogoni Kisiwani Pemba (CUF) akawaomba wajumbe watumie utaratibu wa kura ya kuulizwa mjumbe mmoja mmoja juu ya kuundwa kamati teule na ndipo hapo matokeo ya kura yakatofautiana kutokana na wajumbe wengine wasiokuwa na msimamo wakaogopa ndipo kura 39 walitaka isiundwe kamati teule na waliotaka iundwe ni wajumbe 20 na hivyo suala la kutokuundwa kamati teule likazimika mara moja.

Wajumbe wa baraza la wawakilishi walisimamia hoja yao ya kutaka kuundwa kwa kamati teule ili kuisafisha serikali na kutafuta uoza na tuhuma zilizoelekezwa kwa watendaji juu ya kuwepo uharififu wa fedha kutoka kwa makampuni yalopewa tenda ya kuweka matangazo barabarani ambapo jumla ya makampuni matatu ndio yaliopewa tenda hiyo.

Kwa mujibu wa Waziri Makame anasema kimisingi kuna kosa limetendeka kutoka kwa maafisa wa Manispaa lakini linatokana na hayo makampuni matatu ambayo yanashindana na kila mmoja ametaka kumshitaki mwenzake kwani wamepewa kupashika matangazo barabarani ikiwemo yale ya kampuni za simu za mkononi za zanzitel na tigo lakini kwa mujibu wa Waziri anasema haoni kama huna sababu ya kuunda kamati kuchunguza suala hilo.

Advertisements

7 responses to “Wawakilishi waoga waonekana

 1. wajanja wenye kutetea vibaka wamekutana …… haya …. ndo tunaanza kuamka ..nyie ficheni tu … lkn inshallah vijana tunakuja … kwa uwezo wa Mola tutakuwa sote watu wema…semeni aaaaaaaaaamin… lkn tena acheni hizo nendo … hazina mwisho mwema ..wala mafanikio ya kweli…… yaaalaiti kama mnafahamu haya

 2. ASALAM ALAYKUM!

  Wapi tunaelekea? Kwani ikiundwa hiyo kamati kuna khasara gani? Zimeundwa kamati ngapi na haijakuwa kitu katika upande wa khasara? Anatettewa nani na anaangushwa nani? Anayetetewa aliyobakua na anayeangushwa ni sisi wananchi.

  Kuna haja ya kujipanga upya na watu kuwacha kufanya ushabiki wa vyma Barazani na kukingiana kifua.

  Aonavyo Mzee Shari.

 3. mwizi kila siku atassimama kumlinda na kumtetea mwizi mwenzake,pia tatizo kubwa la wawakilishi wetu uwezo wao mdogo na ndo mana wanashindwa kujiamini,wengine hata kuongea hawajui,mi naskia vibaya hata kuangalia baraza la wawakilishi,some time unamkuta waziri anosoma kwenye note book yake kama mtoto wa standard two,zanzibar hakuna la kuwa tusiongopeane coz bado watu wanafiq

 4. Kwa muono wangu hili suali la kuunda kamati kuchunguza tenda ya kutundika matangazo ni muhimu lakini ni kuliko yalio muhimu ? Kwa sababu limeshawekwa mezani lazima lipewe nafasi yake. Hata hivyo, hatuoni kuwa barazani kumekuwa doro ? Jamani andaeni hoja, baraza likiwa doro hata seriakali inakuwa doro. Mtendaji anachangamshwa kwa wingi wa majukumu yanayotoka kwa wananchi. Mimi sikubaliani na ule usemi kwamba seriali ya pamoja ilioundwa iue upinzani. Kule bungeni nimewahi kuwaona CCM wanapingana wenyewe kwa wenyewe vidole machoni. Kisichowezekana ni mawaziri kivuli tu lakini sio upinzani. Kinacho onekana barazani ni nidhamu ya woga sio kwamba wawakilishi hawana hoja za msingi. Kila mmoja anaogopa kujitokeza aje kuonekana ni tatizo. Aloo, chukueni nafasi yenu kunakucha !!!

 5. Tuorodheshewe Wawakilishi wote waliokataa kuundwa Kamati Teule ya Kuchunguza Ufisadi (KTKU). Nchi ambayo haina Taasisi madhubuti ya kudhibiti ufisadi na wala hakuna Sheria za kudhibiti ufisadi kushindwa alau kuunda KTKU, wakati Mwakilishi ameonesha shaka kuwa kuna ufisadi ni jambo la aibu kwa Wawakilishi wetu. Ingelikuwa ufisadi ni matokeo yanayotokezea mara moja moja nchini Zanzibar tungesema pengine ni shutuma tunazoweza kuzipa muda katika kutafuta ukweli wake bila ya uchunguzi. Lakini nchi imeenea ufisadi kila sehemu ya Serikali, kwanini viongozi wetu wanastahamilia shutuma za ufisadi namna hii? Ni lini watafanya jambo angalau moja litalopeleka ujumbe kwa Mafisadi Serikalini kuwa vitendo vyao hivyo vy hujuma havistahamiliwi tena?
  Kwa maoni yangu Wawakilishi wetu wanaonekana dhahiri kuwa hawana nia ya kuhakikisha ufisadi unadhibitiwa Serikalini. Na hili linaleta taswira mbaya kwa Wananchi ambao wengi wetu tumevunjika moyo na uadilifu wa viongozi wetu. Wengi wao tayari tunawaona ama wao wenyewe ni Mafisadi au wanawasaidia Mafisadi kwa njia moja au nyengine.
  Ole wenu Wawakilishi uchaguzi ujao.Kama leo mnaona haya na woga kuwa labda Mafisadi wachache wa Baraza la Mji watakuoneni wabaya, basi ngojeeni 2015. Sisi wananchi hatutoona haya wala woga, kampeni yetu kila anaeficha Fisadi tutamdhihirisha na tutamtoa.

 6. Aslam aleikum,
  Wewe Khamis Bakar usiharibu mambo wawakilishi wengi ni woga kufukuza kwenye chama kwahiyo kura ni siru iwache iwe siri kwani ndio vizuri hao wezi serikalini wapate kuumbuliwa lakini mukianza kuoneshana vidole kuwa yule kapinga serikari mambo hayatakwenda.

  Nyinyi CUF tuliwategemea sana lakini sasa naona munaanza kuipendelea serikali na kuficha majangili.

 7. hao mawaziri waliokata 39 kuwa tume isiundwa ndio vibaka wenyewe hao na hao kama shein yuko macho anatakiwa awambiye wote wakubali kuchunguzwa na kama hawataki basi wajeuzulu na washatakiwe ndio dawa ya kuwakomesha mawaziri wasiojali haki za wazanzibar na kujali matumbo yao hakuna hili wala lile hao 39 wote hao ndi wakuliza na kuchunguzwa maana ndio washajionyesha kuwa wao ni weziiii thahiriiiiiiiiiii

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s