Tuna vipaumbele vyetu

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,Dk Ali Mohamed Shein,akisalimiana na Balozi wa Canada nchini Tanzania Roert J.Orr,alipofika Ikulu Mjini Zanzibar.

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein amefanya mazungumzo na balozi wa Canada nchini Tanzania Bwana Robert Orr na kumuelezea sekta za maendeleo ambazo zimepewa kipaumbele na serikali anayoiongoza.

Katika mazungumzo hayo, Dk. Shein alimueleza Balozi huyo wa Canada kuwa miongoni mwa sekta za maendeleo ambazo serikali anayoiongoza Dk. Shein imekusudia kuzipa kipaumbele ni sekta ya elimu, afya,kilimo, huduma za kijamii na sekta nyenginezo.

Alisema kuwa serikali ya Mapinduzi Zanzibar yenye muundo wa Umoja wa Kitaifa itaendelea kukuza na kuendeleza maendeleo yaliopatikana nchini katika sekta ya elimu ikiwa ni pamoja na kupambana na changamoto zilizopo.

Alieleza kuwa lengo la serikali ni kufanya elimu ya lazima kuwa kidato cha kumi na mbili ikiwa ni pamoja na kuongeza ubora wa elimu kwa skuli za sekondari na msingi na kuhakikisha watoto wote waliofikia umri unaostahiki wanapatiwa elimu hiyo.

Dk. Shein alimueleza Balozi huyo kuwa serikali ina malengo ya kuimarisha mafunzo ya waalimu kwa kuwapatia elimu bora ili nao waweze kutoa mafunzo mazuri kwa wanafunzi wao. Aidha, alisema kuwa kipaumbele chengine katika sekta hiyo ni kuhakikisha waalimu na wahadhiri wanajengewa uwezo mkubwa kutoa mafunzo.

Pia, Dk. Shein alimueleza balozi huyo kuwa miongoni mwa mipango inayoendelezwa ni kujenga skuli mpya za sekondari pamoja na nyumba za waalimu Unguja na Pemba.

Akizungumzia kuhusu sekta ya afya, Dk. Shein alisema kuwa tayari sekta hiyo imepata mafanikio makubwa na hatua iliyopo hivi sasa ni kuiimarisha zaidi sekta hiyo ili kuhakikisha inatoa huduma bora kwa jamii ikiwa ni pamoja na kuifanya hospitali ya ManaziMoja kuwa ya kiwango cha hospitali ya rufaa kwa kuipatia vifaa vya kisasa na wataalamu.

Alieleza kuwa hatua zimechukuliwa katika kutafuta vifaa vya kisasa vya uchunguzi wa maradhi sanjari na kuwapatia mafunzo madaktari wa hapa nchini kuwa mabingwa katika fani mbali mbali kwa lengo la kuwapatia wananchi matibabu hapa hapa nchini.

Pamoja na hayo, Dk. Shein alieleza kuwa lengo la serikali ni kuzipandisha daraja hospitali za Wilaya kuwa hospitali za Mkoa . Aidha, hospitali zilizo kiwango cha ‘cottage’ zikiwemo Micheweni na Vitongoji Pemba na Makunduci na Kivunge za Unguja.

Dk. Shein pia, alimueleza Balozi huyo kuwa hatua pia zinachukuliwa katika kupambana na maradhi mbali mbali yakimwemo Malaria, Ukimwi pamoja na maradhi mengine sugu na kusisitiza kuwa tatizo la vifo vya akina mama na watoto pia, ni miongoni mwa juhudi zinazochukuliwa katika kuhakikisha linapungua ama kuondoka kabisa.

Katika sekta ya kilimo, Dk. Shein alieleza kuwa kilimo ni sekta muhimu na pia, ni uti wa mgongo kwa Wazanzibari walio wengi kwani zaidi ya asilimia 50 wanajishughulisha na sekta hiyo lakini bado kilimo chao wanatumia zana za asili ikiwa ni pamoja na kutegemea mvua.

Kutokana na hatua hiyo, Dk. Shein alieleza kuwa serikali anayoiongoza ina mpango wa kutilia mkazo kilimo cha umwagiliaji maji tayari kuna mabonde 57 yenye hekta 8,521 ambazo zinaweza kutumika kwa kilimo hicho.

Ambapo hadi sasa kwa maelezo ya Dk. Shein jumla ya hekta 700 za eneo hilo zimeshajengewa miundombinu ya umwagiliaji huku serikali ikiendelea na matayarisho ya mradi mkubwa wa kilimo cha umwagiliaji kwa msaada wa serikali ya Jamhuri ya Korea ambapo jumla ya hekta 2000 zimeshatayarishwa.

Akieleza juu ya suala zima la utafiti, Dk. Shein alisema kuwa serikali inampango wa kuimarisha shughuli za utafiti utakaohusisha mbegu bora. Aidha, Dk. Shein alitoa shukurani kwa misaada inayotolewa na nchi hiyo kwa Zanzibar.

Dk. Shein pia, alimueleza Balozi huyo kuwa amani na utulivu inaendelea kupatikana hapa nchini kutokana na wananchi wenyewe kuwa wamoja na kushirikiana katika kuiletea nchi yao maendeleo.

Nae, Balozi wa Canada bwana Orr, alimueleza Dk. Shein kuwa nchi yake itaendelea kuiunga mkono Zanzibar katika kufikia malengo yake yaliyokusudia na kusifu amani, utulivu na mshikamano mkubwa uliopo nchini chini ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar yenye muundo wa Umoja wa Kitaifa.

Balozi huyo alieleza kuwa atahakikisha Zanzibar inafaidika na misaada inayotolewa na nchi hiyo ikiwa ni pamoja na misaada ya elimu, misaada ya kifedha na misaada ya kusaidia uimarishaji wa sekta nyenginezo za maendeleo.

Aidha, Balozi Orr alieleza kuwa kutokana na mafanikio yaliopatikana Zanzibar katika uimarishaji wa sekta ya utalii na uwekezaji juhudi atachukua katikakuitangaza Zanzibar nchini mwake na kusifu mikakati iliyowekwa na serikali anayoiongoza Dk. Shein katika kuimarisha sekta za maendeleo.

Sambamba na hayo, balozi huyo alitoa pomgezi kwa mafanikio yaliopatikana Zanzibar kwa kufanya uchaguzi uliokuwa huru na wa haki na uliofanyika kwa amani na utulivu mkubwa na kusisitiza kuwa nchi yake itaendeleza ushirikiano na uhusiano wake na Zanzibar.

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s