Nitawashitaki nitakapopumzika

Jaji Mkuu wa Zanzibar Hamid Mahmoud akiongea na waandishi wa habari muda mfupi baada ya sherehe ya kuwaapisha Mahakimu wapya wa Wilaya na Mkoa, Vuga Mkoa wa Mjini Magharibi Zanzibar

 JAJI MKUU wa Zanzibar Hamid Mahmoud amewashukia Chama Cha Wanasheria Zanzibar (ZLS) na Gazeti la Mwanahalisi kutokana na kumfuata fuata katika utendaji w akazi zake na kuandika kwamba kumaliza muda wake na kazi.

Alisema yeye bado hajamaliza na leo (Aprili mosi anaanza mapumziko ya kustaafu hadi Aprili 30) jambo ambalo amesema ni la hiyari na sio kulazimishwa na mtu huku aksiema kustaafu kwake kunatokana na afya yake.

“Napumzika mwenyewe kutokana na afya yangu hivi sasa naumwa na uti wa mgongo kutokana na kukaa muda mrefu katika kiti nikiwa kazini lakini sio kama wanavyosema hao chama cha wanasheria au kama ilivyoandika gazeti la mwanahalisi” alisema Jaji huyo.

Kauli ya Jaji Mahmoud imekuja muda mfupi baada ya kumaliza kuwaapisha mahakimu wa wilaya katika sherehe za viapo hiyo iliyofanyika katika Mahakama ya Mkoa Vuga leo ambapo alisema chama hicho ni cha wababaishaji hivyo aliahidi kuwafikisha mahamakani wakati anapokuwa mstaafu pamoja na gazeti la Mwanahalisi ambalo limeandika habari isiyo na ukweli huku akitoa angalizo la kulitaka kumuomba radhi na ikishindakana atalifikisha mahakamani na atadai fidia anayotaka mwenyewe.

Jaji Mahmoud alisema Chama Cha Wanasheria pia kitafute pesa katika chama cha siasa kinachowatuma kumsakama yeye kwa ajili ya kumlipa fidia pindi akiwafikisha mahakamani wakati ukifika kwa kuwa amekuwa akisakamwa na chama hicho mara kwa mara kutokana na nafasi yake aliyonayo.

Aidha alisema chama cha wanasheria wamekurupuka na wanahaha sana, kwa sababu kifungu cha 95 (3) kimeeleza licha ya kuwa jaji amefika umri ulioainisha jaji wa mahakama kuu ataendelea katika wadhifa wake huo mpaka pale atapomaliza shughuli zote ambazo zilimfikia kabla ya kutimiza umri huo.

 alisema kutokana kukosa kukijua kifungu hicho wamekurupuka na kusambaza mabarua kwa vyombo vya habari na sehmeu nyengine lakini yeye anaondoka katika wadhifa wake huo kifua mbele bila ya kuwa na chembe ya khofu.

Jaji Mahmoud aliwapisha Mrajis wa Mahakama Kuu Zanzibar, Joseph Kazi, Mahakimu wa Mkoa Khamis Ali Simai na Said Hemed Khalfan pamoja na Mahakimu wa Wilaya ni pamoja na Mbarouk Nassor Mbarouk, Ali Abdulrahman Ali, Omar Mcha Hamza, Valentina Andrew Katema, Fatma Muhsin Omar, Rashid Machano na Sabra Ali Mohammed.

 Aidha aliwataka nasaha zake kwa watendaji hao aliwapongeza kwa kupata wadhifa hizo, na kuwambia kuna changamoto nyingi wanazowe kukabiliana nazo kutokana na ugumu wa kazi hiyo. Aliwashauri wafanyekazi kwa kusaidia maendeleo ya mahakama ili shughuli za Serikali ziende vizuri katika kuhakikisha haki inapatikana.

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s