Habari za Brazil salama huko?

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein,akisalimiana na Balozi wa Brazil Nchini Tanzania,Fransisco Carlos,alipofika Ikulu Mjini Zanzibar

SERIKALI ya Japan imeahidi kuendelea kuiunga mkono Zanzibar kwa kuiongezea nguvu zaidi  Mamlaka ya Maji Zanzibar (ZAWA), ili  kuhakikisha  hatua iliyofikiwa katika mradi mkubwa wa maji Mjini Unguja inaendelezwa kwa lengo la kuwapatia wananachi huduma hiyo.

Balozi wa Japan nchini Tanzania  Mhe. Hiroshi Nakagawa aliyasema hayo leo wakati alipokuwa na mazungumzo na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein Ikulu mjini Zanzibar.

 

Katika mazunguzmo hayo, Balozi Nakagawa alimueleza Dk. Shein kuwa  Japan itaendelea kutoa ushirikiano wake mkubwa katika kuhakikisha inaiunga mkono Zanzibar katika kuimarisha sekta zake za maendeleo.

 

Bwana Nakagawa alirejea msimamo wa  nchi hiyo kwa Zanzibar kuwa licha ya uharibifu mkubwa na maafa yaliotokezea nchini mwake lakini nchi hiyo itaendelea kuisaidia Zanzibar na kuahidi kutimiza ahadi zote inazoahidi nchi hiyo kwa Zanzibar.

 

Pamoja na hayo, Balozi huyo alimueleza Dk. Shein kuwa Mashirika mbali mbali ya nchi hiyo yanayotoa misaada nayo yataendelea kuiunga mkono Serikali ya Mapinduzi Zanzibar likiwemo Shirika la JICA na mengineyo.

 

Aidha, Balozi huyo alimueleza Dk. Shein kuwa anamatumaini makubwa kuwa mkataba uliotiwa saini hivi karibuni ambao Japan utaisaidia Zanzibar zadi ya  Shilingi Bilioni 52  za Kitanzania kwa ajili ya mradi wa kusambazia umeme hapa nchini.

 

Alisema kuwa Serikali ya Japan imekuwa ikiiunga mkono Zanzibar katika kuimarisha sekta mbali mbali za maendeleo kwa lengo la kuhakikisha wananchi wa Zanzibar wananufaika na huduma zinazotokana na sekta hizo.

 

Balozi huyo pia, aliendelea kutoa  pongezi zake na kwa nchi yake ya Japan kwa Dk. Shein pamoja na wananchi wote wa Zanzibar kwa  kufanya uchaguzi mkuu uliopita kwa amani na utulivu mkubwa.

 

Nae Rais Dk. Shein ameeleza kuwa hatua ya Japan kuahidi kutoa ushirikiano wake katika kuiongezea nguvu Mamlaka ya Maji Zanzibar (ZAWA), itasaidia kwa kiasi kikubwa kuendeleza juhudi za serikali katika kuhakikisha wananchi wake wote wanapata huduma hiyo muhimu ya maji.

 

Dk. Shein alisema kuwa awamu zote mbili za mradi huo zimeenda vizuri na kubwa lililobaki hivi sasa ni tatizo la kuweza kusambaza huduma hiyo mitaani ili kuwafikia wananchi, hiyo ni kutokana na uchakavu wa miundombinu ya kusambazia.

 

Alieleza kuwa kutokana na serikali kuelewa tatizo hilo  linalowakabili wananchi kwa baadhi ya maeneo ya mji wa Unguja, juhudi za makusudi za kuwapelekea wananchi huduma hiyo ya maji mitaani kwa kutumia magari huchukuliwa ili kuwarahisishia wananchi kupata huduma hiyo.

 

Aidha, Dk. Shein alitoa shukurani kwa serikali ya Japan kutokana na msaada mkubwa  wa fedha uliotoa kwa Zanzibar kwa ajili ya mradi wa kusambaza umeme na kueleza kuwa kiasi hicho cha fedha ni kikubwa na hiyo ni kutokana na Japan kutahini uhusiano na ushirikiano uliopo kati ya nchi mbili hizo.

 

Alieleza kuwa kukamilika kwa mradi huo wa umeme hautosaidia huma ya majumbani pekee bali utasaidia hata katika kukuza sekta nyengine za maendeleo na kuimarika kwa uchumi hapa Zanzibar.

 

Pamoja na hayo, Dk. Shein alimueleza Balozi huyo kuwa Zanzibar inathamni misaada na ushirikiano wa Japan ikiwa ni pamoja na kuimarisha sekta za maendeleo hapa nchini na kueleza kuwa wananchi wa Zanzibar wako pamoja na ndugu zao wa Japan hasa katika kipindi hichi ambacho nchi hiyo imepata janga kubwa.

 

Wakati huo huo, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein alifanya mazungumzo na Balozi wa Brazil nchini Tanzania ambapo katika mazungumzo hayo, viongozi hao walizungumzia juu ya kuendeleza ushirikiano katika sekta za maendeleo zikiwemo kilimo, elimu, utalii, umeme, michezo na utamaduni.

 

Katika mazungumzo hayo Dk. Shein alimueleza Balozi huyo kuwa Zanzibar ina mengi ya kujifunza kutoka Barazil na kusisitiza haja ya mashirikiano katika sekta ya elimu pamoja na kujenga uhusiano baina ya vyuo vikuu vya nchi hiyo na Chuo Kikuu cha Taifa Zanzibar (SUZA), ikiwa ni pamoja na kubadilishana wataalamu.

 

Aidha, viongozi hao walizungumzia umuhimu wa uhusiano katika suala zima la utafiti kati ya taasisi na vyuo vikuu vya Brazil na Zanzibar ambao utaweza kuwakutanisha wataalamu wa tafiti mbali mbali zikiwemo za kilimo na kuweza kukaa pamoja na kujadiliana juu ya tafiti hizo.

 

Balozi wa Brazil nchini Tanzania  bwana  Fransisco Carlos naye kwa upande wake alimueleza Dk. Shein kuwa nchi yake inathamini uhusiano wa muda mrefu kati yake na Zanzibar  na kueleza kuendelea kutoa ushirikiano wake.

 

Aidha, Balozi huyo wa Barazil alimueleza Dk. Shein kuwa nchi yake imeandaa mradi maalu wa kusaidia vifaa vya michezo kwa ajili ya vijana, wakiwemo mayatima na wale walioathirika na virusi vya ukimwi. Pamoja na hayo, viongozi hao wamezungumzia lengo la kushirikiana pamoja katika kuimarisha sekta ya michezo hapa nchini.

 

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s