Umeme wasimamisha vikao

Jengo la Baraza la Wawakilishi Zanzibar ambalo kwa leo limeshindwa kuendesha vikao vyake kutokana na ukosefu wa umeme katika jengo hilo

Wajumbe wa baraza la wawakilishi Zanzibar leo wameshindwa kuelendelea na kikao vyao vinavyopaswa kuendelea nyakati za asubuhi na jioni kutokana na tatizo la ukosefu wa umeme katika jengo hilo la baraza ambalo umeme huo umekuwa ukikatika mara kwa mara katika maeneo yote ya hapa Zanzibar, shida ya ukosefu wa umeme imekuwa ni tatizo sugu kwa hapa Zanzibar kama ilivyo tatizo la maji ambapo kumekuwepo na kauli zisizofahamika juu ya tatizo la ukosefu wa umeme wakati baadhi ya maafisa wa Shirika la Umeme Zanzibar (ZECO) wakisema tatizo hilo ni la muda mfupi lakini maafisa wa shirika hilo hilo wengine wanasema kwamba kutahitajika muda katika suala hilo na kuzimwa umeme.

Wakati Tanzania bara wanatumia umeme wa mgao Zanzibar nayo kumekuwepo na umeme wa mgao lakini ni tofauti na kwa masaa Tanzania bara huchukua muda mrefu lakini Zanzibar huzimiwa umeme kwa muda wa saa moja kwa kila eneo ambalo huzimwa. Baraza jipya la wawakilishi lina viyoyozi (AC) zaidi ya kumi katika ukumbi wa wajumbe unashindwa kuwasha jenereta walilonalo kutokana na jenereta walilonalo halina ngvu za kutosha kuwashia viyoyozi hivyo.

Wananchi wa Zanzibar wamekuwa na maswali mengi ya kuuliza juu ya tatizo hilo la ukosefu wa umeme na wakirudi nyuma kuyakumbukia yale majenereta ya dharura ambayo yalizinduliwa julai 29 mwaka 2010 ambapo rais msataafu Amani Abeid Karume alikuwa mgeni rasmi katika hafla hiyo iliyowakusanyisha maafisa wa ubalozi wa  kutoka nchi mbali mbali za ulaya ambazo ni wafadhili pamoja na wananchi mbali mbali wa Zanzibar.

Jumla ya majenereta 32 ya kuzalisha umeme wa dharura yalifungwa kwa mashirikiano ya serikali ya Uingereza, Norway na Sweeden na serikali ya Mapinduzi Zanzibar zimetoa jenereta hizo zenye uwezo wa kuzalisha umeme wa (IMVA) na ambazo zinatumia mafuta ya dezeli.

Msaada huo umelikuwa umekuja kwa wakati muafaka kutokana wakati huo Zanzibar ilikuwa tayari imekubwa na tatizo la ukosefu wa umeme kwa miezi mitatu mfululizo na kuathiri uchumi wa Zanzibar kwa kiasi kikubwa khasa kwa kuwa Zanzibar inategemea shughuli za kibiashara lakini pia kazi nyingi na zilidorora ikiwmeo taasisi zenye kutoa huduma za kijamii ziikuwa zimesitisha kutoa huduma na nyengine zikisuasua kutokana na tatizo hilo.

Kwa mujibu wa wahisani wa maendeleo ambao wamefadhili majenereta hayo walisema wakati wa uzinduzi huo uliofanyika Mtoni nje kidogo ya mji wa Zanzibar, gharama za ununuzi wa majenereta hayo na kuzifunga ni takriban shilingi 17 billioni za kitanzania na walisema zitakuwa na uwezo wa kuzalisha megawati 25.

Mchanganuo unaonesha kwamba gharama za jumla, ukijumuisha na ununuzi, usafirishaji, kuzifunga na nguvukazi ni takriban shilingi 19 billioni fedha za kitanzania.Katika kiasi hicho Norway, Sweeden na Uingereza zimetoa shilingi 17 billioni wakati serikali ya mapinduzi Zanzibar ikijazia 1.7 billioni.

Taarifa inaweka bayana kwamba Swedeen ilitoa mchango huo kwa kutumia Shirika la Misaada la Kimataifa (SIDA) wakati Uingereza imetumia Idara ya Misaada ya Kimataifa (DFID)

Wafadhili siku ya uzinduzi walisema kwamba majenereta hayo ya umeme wa dharura yatatoa unafuu mkubwa kwa watu wanaokadiriwa kufikia laki nane (800,000) wa Zanzibar.

Sehemu ya taarifa ya wafadhili iliongeza kwamba umeme huo utakuwa nafuu kwa idadi hiyo ya watu kwa kujumuisha asilimia 25 ya mitaa ambayo imeunganishwa na gridi ya taifa.

Zanzibar ilikubwa na tatizo kubwa la umeme baada ya kuharibika njia kuu za kufikishia umeme kutoka kiromoni hadi fumba kituo kikuu cha kupokea umeme kutoka gridi ya taifa mwaka 2009. tatizo hilo lililodumu kwa miezi mitatu liliathiri sekta ya biashara baada ya wafanyabiashara kutakiwa kufanya kazi kwa saa chache na maeneo mengine kufungwa kabisa kutokana na kukosekana kwa nishati hiyo.

Hali hiyo pia iliathiri mfumo wa usambazaji wa maji safi ambayo kwa tathimini ya umoja wa mataifa (UN), tatizo hilo lilipunguza usambazaji maji safi kwa asilimia 50. serikali ya mapinduzi pia ililazimika kutumia fedha nyengine za ziada kwa ajili ya kuziba pengo hilo. Jenereta hizo mpya zilitarajiwa kuwa chanzo kipya cha umeme wa dharura wa Zanzibar.

jambo ambalo limekuwa likisumbua katika taasisi nyingi na baadhi ya wananchi wanaokosa umeme huyo kutokana na kuwepo mgao maalumu hapa Zanzibar, lakini wananchi wanauliza yale majenereta yaliogharimu mabillioni ya shilingi kwa nini hayatumiki wakati huu wenye kujua kusema wanasema hivi kuendesha majenereta yale ni gharama, sasa swali lipo hivi kama mlijua ni gharama kwa nini mlikubali kugharamikia kitu msicho na uwezo nacho?

Advertisements

One response to “Umeme wasimamisha vikao

 1. Umeme kutoweka

  Hivi sasa katika suala zima la Mabadiliko ya hali ya hewa ni kutumia nishati mbadala, nishati ambayo ni rafiki kwa Mazingira na vilevile ni yenye gharama nafuu.

  Nathubutu kusema kuwa nimefarajika Umeme huo kuzimika kwenye jengo letu hili la watunga Sheria. Kwani hapo wataweza kutafakar na kama wataalamu wanaposema wataweza kufahamu.

  Safari mmoja nilikuwa nasoma juu ya Umeme unaotokana na Nishati ya Jua, nikaona gharama za kuanzia namna zinavyokuwa kubwa na mwishowe mtu kujikuta kama anageiwa Umeme bure.

  Baraza la Wakilishi linahitajia kuwa na umeme mbadala wala sio generator, mashine za generator ni ghali kutumia kwani mafuta tunayapandisha bei wenyewe.

  Tukae na kutafakari.

  Wakatabahu

  Mzee Shari

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s