udhibiti wa maadili ni kazi kubwa

Waziri wa Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo, Abdillah Jihad Hassan

SERIKALI ya Mapinduzi ya Zanzibar imesema licha ya kuwa suala la mporomoko wa maadili ni gumu kudhibitiwa kutokana na kukua kwa sekta ya utalii lakini imewataka wananchi kujaribu sana kufuata maadili ya dini yao na kuwakataza watoto wao kufuata mila na tamaduni za nchi nyengine.

Akijibu maswali katika kikao cha baraza la wawakilishi Mjini hapa, Waziri wa Habari Utamaduni, Utalii na Michezo, Abdillahi Jihadi Hassan aliloulizwa na Mwakilishi wa Jimbo la Chambani (CUF) Mohammed Mbwana Hamad aliyetaka kujua serikali ina mpango gani wa kudhibiti mporomoko wa madili unaosababishwa na utalii.

“Kwa kuwa utalii ambao ni miongoni mwa vyanzo muhimu vya uchumi wa Zanzibar umekuwa ukisababisha mporomoko wa maadili mazuri ya Zanzibar kutokana na watalii wengi wanaoingia nchini kinyume na maadili hayo na silka za Zanzibar jee serikali ina mpango gani wa kuchukua hatua madhubuti na zinazotekelezeka, kuhakikisha hali hiyo na mporomoko wa maadili inadhibitiwa?” alihoji Mwakilishi huyo.

Waziri Jihadi alisema serikali inachukua juhudi za kudhibiti suala hilo na kwa kuwa utalii uemingia nchini kwa kazi kubwa imekuwa sio kazi rahisi kuhibiti maadili na silka za wazanzibari kwa haraka.

Hata hivyo amesema hakuna uchahidi kwamba ni sekta ya utalii tu ndio inayopelekea mporomoko wa maadili utamaduni na silka lakini ni wazi kuwa utandawazi ni chanzo kikuu cha mporomoko wa maadili na silka za wazanzibari.

Hata hivyo waziri huyo aliwaambia wjaumbe wa baraza la wawakilishi kwamba hatua mbali mbali zinachukuliwa na kamisheni ya utalii, umaduni na michezo ili kutatua tatizo hilo kutokana na kwamba sekta hiyo imemilikiwa na watu binafsi ambao wanazingatia zaidi maslahi yao ya biashara kuliko maadili na silka za nchi.

Pamoja na hali hiyo serikali imekuwa ikijitahidi kuthibiti mporomoko wa maadili na silka na utamaduni katika namna tofauti ikiwemo kuzidisha ushirikiano uliopo kati ya kamisheni ya utalii Zanzibar na kamisheni ya utamaduni katika kuhakikisha kuwa hatua madhubuti zinachukuliwa ili kurudisha hadhi ya maadili ya wazanzibari.

Alisema kupitia mpango wa utekelezaji wa kazi wa kamisheni ya utamaduni, Serikali inaendeleza tamasha la utamaduni wa Mzanzibari kila mwaka kwa makusudi ya kuelimisha jamii juu ya maadili na silka njema za Kizanzibari  kwa wenyeji na wageni kutoka nje ya nchi.

Waziri huyo alisema katika kudhibiti maadili na silka za mzanzibari Kamisheni ya utamaduni inaendelea kutumia vyombo vyake vya kiutendaji ambavyo ni baraza la utamaduni na sanaa kwa kutoa elimu juu ya umuhimu wa kulinda maadili ya hapa Zanzibar.

Aidha alisema baraza la Kiswahili, bodi ya sensa ya Filamu na sanaa za maonyaesho kwa ajili ya kuulinda kuelimisha kuenzi na kuendeleza utamaduni wa mzanzbari ambao ni rasilimali kubwa ya nchi.

Tatizo la mporomoko wa maadili hivi sasa limekuwa kwa kiasi kikubwa ambapo baadhi yam sheikh na maulamaa wameitahadharisha jamii kuweza kukabiliana nayo huku wakiitaka serikali kuchukua hatua madhubuti ya kukabiliana na tatizo hilo.

Vijana wengi wa kizanzibari wamekuwa wakijiingiza katika mambo ya kuiga utamaduni wa kimagharibi ambapo baadhi ya vijana wameacha mila na tamaduni zao na kufuata maadili ya nje jambo ambalo limekuwa likiathiri mila na tamaduni za Zanzibar.

Awali baadhi ya wajumbe wa baraza la wawakilishi waliishauri serikali kurudi nyuma na kuweka masharti maalumu ya kulinda maadili kama ambavyo rais na muasisi wa Zanzibar, Marehemu Mzee Abeid Amani Karume alivyokuwa akilinda mila na utamaduni wa mzanzibari alipokuwa akiweka utaratibu maalumu kwa kudhibiti uharibifu wa maadili kwa kuweka masharti ya nguo zenye kufuata maadili ya Zanzibar kwa wageni wote wanaoingia nchini.

Hata suala hilo linaonekana kutofanya kazi kwa sasa kutokana na Tanzania kusaini azimio la haki za binaadamu ambapo baadhi ya wajumbe walisema kumpangia mtu nguo ya kuvaa hapa nchini ni kukiuka mashati ya azimio hilo na ni uvunjani wa haki za binaadamu kuweka masharti kama hayo.

MWISHO

BAADHI ya wajumbe wa baraza la wawakilishi wameishauri Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kuuweka katika ratiba ya serikali mwaka wa kiislamu na kuifanya siku hiyo kuwa ni ya mapunmziko kwa wafanyakazi hapa Zanzibar.

Ushauri huo umetolewa na baadhi ya wajumbe ambapo awali Mwakilishi wa Jimbo la Muyuni (CCM) Jaku Hashim Ayoub alipouliza kwani nini siku hiyo isiwekwe kama ni siku ya mapumziko na kuingizwa katika ratiba maalumu za kiserikali.

“Ni dhahiri kuwa wazanzibari tulio wengi ni waislamu tunakubali pia kuwa uislamu ni mfumo mzima wa maisha yenye mila zake na desturi zake, khulka zake na sherehe zake lakini kama zilivyo mila desturi silka na khulka nyengine mambo hayo yanahitaji kutunzwa na kuadhimishwa, jee mheshimiwa waziri wizara yako haioni kuwa katika kuzienzi mila desturi, silka na khulka za kiislamu kuwa haja ya kuadhimisha kuanza kwa mwaka wa kiislamu na kuifanya siku hiyo kuwa ya mapumziko hapa Zanzibar?” alihoji Ayoub.

Akijibu swali hilo Waziri wa kaiba na sheria, Abubakar Khamis Bakari alisema kimsingi anakubali na na muuliza swali kwamba wazanzibari welio wengi ni waislamu na pia anakubaliana naye kwamba upo umuhimu wa kuzienzi mila, desturi na silka za kiislamu kwa vile ni mfumo mzima wa maisha ya kila siku ya wazanzibari walio wengi.

“Uislamu unazo sikuu mbili rasmi nazo ni eid el fitri na eid al hajj kwa utukufu wa mazazi ya Mtume Muhammad (s.a.w) siku hiyo pia inatambuliwa rasmi ni siku ya sikukuu” alisema Waziri huyo.

Hata hivyo alikiri kulingalia kwa undani zaidi suala hilo la mwezi moja muharam kwa hivyo wizara yake itafanya utafiti kwa kupitia sheria za kiislamu na kwa kutazama jitihada za maulamaa ili wizara ipate kuwa na uwezo wa kuishauri serikali kwa vizuri na kwa ustawi kuhusu kuifanya siku ya mwezi mosi muharram kuwa siku kuu ya kitaifa.

Aliwaambia wajumbe wa baraza la wawakilishi kwamba wizara inaahidi kufanya hivyo kwa kushirikiana na ofisi ya makamu wa pili wa rais kwa sababu hiyo ndio wizara inayohusika na sikuu za serikali.

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s