Tumepiga hatua kidogo

Waziri wa Nchi Afisi ya Rais Fedha, Uchumi, na Mipango ya Maendeleo, Omar Yussuf Mzee akizindua ripoti ya utafiti wa kibiashara uliofanywa na taasisi ya kimataifa ambayo ni ya kwanza kutolewa na Benki ya Dunia katika hoteli ya Bwawani Mjin Zanzibar

 

IMEELEZWA kwamba Zanzibar imeshika nafasi 155 katika utafiti wa kibiashara uliofanywa na taasisi moja ya kimataifa chini ya ufadhili wa benki ya dunia.

Meneja wa kanda ya mashariki na kusini mwa Afrika na muwekezaji mshauri wa benki ya dunia (IFC), Peter Ladegaard alisema mchakato huo ulizishirikisha nchi 183 ambapo Zanzibar iliibuka na nafasi hiyo ya 155.

Ripoti hiyo ni ya kwanza kutolewa na Benki hiyo kwa utafiti wa eneo la biashara ambapo ilizinduliwa rasmi na Waziri wa Nchi Afisi ya Rais Fedha, Uchumi, na Mipango ya  Maendeleo  Omar Yussuf Mzee.

Wakizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa hoteli ya Bwawani juzi wamesema hiyo ni faraja kwa Zanzibar kupata nafasi kama hiyo ambapo mkazo wa utekelezaji utaongezwa ili Zanzibar iweze kupata nafasi nzuri zaidi.

Mtaalamu huyo alisema utafiti huo kwa upande wa Zanzibar uliangalia zaidi mazingira ya Zanzibar kuhusu  uendeshaji biashara kisheria ambao ulianza kufanyika  Machi 22, mwaka jana, na kubainisha kwamba bado Zanziba  ipo mahali pazuri ikilinganishwa na Tanzania bara kwa vile imeshika nafasi ya 182

Akizungumzia mikataba ya kibiashara, Ladegaard, katika utafiti huo alisema kuwa Zanzibar imeshika nafasi ya 37 kati ya 183 ikiwa ya pili katika nchi 34 za visiwa vidogo vyenye kuendesha biashara.

Aidha utafiti huo ujmebaini wafanyabiashara katika maeneo ya mijini  umebaini kuwa ni yenye kufikiwa kirahisi na wafanyabiashara wake ikilinganishwa na Tanzania Bara.

Kuhusu upatikanaji wa vyanzo vya biashara umebainisha kuwa hali ni nzuri kutokanana uhusiano wa karibu kati ya wafanyabiashara na wateja wao, huku ulipaji hawendi kwa kasi kutokana na kuwepo vyombio vingi vinavyofanyakazi ya aina moja.

Aidha, mtaalamu huyo kasoro moja wapo kubwa iliobanika kwenye utafiti huo ni kuanza kupungua kumbukumbu za biashara zinazoingizwa kutoka nje ya Zanzibar, lakini ukabainisha kwamba sekta binafsi ndio tegemeo kubwa la ajira Zanzibar kuliko sekta ya umma.

Kutokana na  kasoro zilizojitokeza, mtaalamu huyo ameshauri ushirikiano uimarishwe  kati ya baraza la biashara na sekta binafsi ili kama changamoto ya kukua kwa sekta ya ajira.

Naye Katibu Mkuu wa Wizara Nchi Afisi ya Rais Fedha, Uchumi, Mipango ya  Maendeleo,  Khamis Mussa Omar , alisema kuwa serikali baada ya kupokea ripoti hiyo itakaa  biashara jambo ambalo liliifanya mazingira yake kushindwa kwa serikali kuendelea nayo.

 Waziri wa wizara hiyo Omar Yussu Mzee amesema kuwa utafiti huo utaipa Zanzibar changamoto kuweza kuweka mazingira bota ya kibiashara ambayo yatasaidia kuleta mabadiliko.

Alisema historia ya Zanzibar imejengwa kwa misingi ya biashara ambapo hadi mwaka 1980 biasahara ilikuwa ikiendeshwa zaidi na serikali kwa kuagiza bidhaa kutoka nje zaidi lakini 1994 iliamua kuwachia shughuli hizo kufanywa zaidi na watu binafsi.

alisema kutokana na utafiti huo ni wazi kuwa tayari umeweza kuyaona maeneo mapya ya kufanya sekta ya biashara kuwa imara zaidi ambapo serikali itahakikisha inayafania kazi kutokana na kuwa hivi sasa ni moja ya sekta muhimu inayoweza kuongeza viwango vya ajira.

Advertisements

One response to “Tumepiga hatua kidogo

  1. Tuna unga mkono jitihada zote ambazo serekali imeazimia kuzichukua na kuhakikisha nchi inasonga mbele na inapiga hatua kubwa za kimaendeleo kwa lengo la nchi na wananchi wake,kuhakikisha biashara inashika kasi na kuwepo mzunguko mzuri kibiashara

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s