Watatusaidia wahisani

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi akisalimiana na Waziri wa Biashara, Viwanda na Masoko, Nassor Ahmed Mazrui na baadar Waziri asiye na wizara maalumu, Machano Othman Said baada ya kumaliza kuzungumza na waandishi wa habari alipowasili katika uwanja wa ndege wa Zanzibar muda mfupi baada ya kurudi safari yake ya Nchini Iran alipokwenda kuhudhuria tamasha la utamaduni Machi 26, ambapo alipata fursa ya kuongea na Rais wa Iran na kuahidi kuisaidia Zanzibar katika sekta ya elimu na afya.

SERIKALI ya Mapinduzi ya Zanzibar imeahidi kupeleka wataalamu wa fani mbali mbali nchini Iran, kama ni hatua ya kufuatilia utekelezaji wa mambo yalioafikiana kati ya nchi mbali hizo zenye uhusiano mzuri.

Kauli hiyo imetolewa na Makamu wa Pili wa Rais, Balozi Seif Ali Iddi, jana wakati akizungumza na waandishi wa habari uwanja wa ndege wa Zanzibar alipowasili nchini akitokea nchini Iran kwa ziara yake ya siku tatu kiserikali ambayo pamoja na mambo mengine alihudhuria maonesho ya utamaduni wa nchi hiyo.

Iddi alifanya ziara hiyo kumuwakilisha Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohammed Shein aliyealikwa na Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran, Rais Mahmoud Ahmadinejad.

Tatizo baadhi ya maafisa wa serikali kutofuatilia makubaliano yaliofikiwa kati ya Zanzibar na nchi wahisani limeelezwa ni kubwa ambapo hivi karibuni akizungumza na waandishi wa habari baada ya ziara yake ya kiserikali, Makamu wa kwanza wa rais Maalim Seif Sharif Hamad alisema kuna tatizo hilo nchi zinapokubaliana miradi maafisa wanashindwa kufuatilia jambo ambalo ameahidi kulichukulia kwa umakini mkubwa.

Mbali na kushiriki katika tamadha hilo la utamaduni lakini Balozi pia alipata fursa ya kuonana na viongozi mbali mbali wa nchi hiyo ambapo Zanzibar imepata kujifunza mambo mengi juu ya tamasha hilo.

Alisema kimsingi mahusiano yaliopo kati ya Zanzibar na Iran ni mazuri na viongozi wote wamahihidi kudumisha mahusiano hayo na kuyaendeleza kwani wananchi wa nchi mbali hizo ni ndugu kwa muda mrefu.

Alisema jambo kubwa ambalo serikali ya Zanzibar itaweza kufaidika nalo ni kuona inaandaa timu maalum ya wataalamu ambayo itakwenda nchini humo kwa ajili ya kukamilisha makubaliano ya kisekta yaliofikiwa na pande mbili hizo.

Balozi seif alisema wameamua kuchukua hatua hiyo ya kwanza ambayo serikali itaichukua baada ya kuona kuwepo kwa udhaifu wa mengi ya makubaliano yaliofikiwa yameshindwa kufuatiliwa katika awamu iliyopita.

Alisema serikali ya Iran na serikali ya Zanzibar katika miaka iliyopita iliweza kuwa na mikataba na nchi ya Iran lakini hadi sasa bado haikutekelezwa ambapo hivi sasa serikali itatuma timu yake haraka kufanikisha hilo.

Akiitaja baadhi ya mikataba hiyo Balozi Iddi alisema ni pamoja na mikataba inayohusu sekta ya afya na mengine ni ya kiuchumi.

Hata hivyo Balozi Idd, alisema licha ya kuwepo hilo pia serikali imewakaribisha wawekezaji wa Irani katika sekta ya Afya kuja Zanzibar kujenga Hosptali ya kisasa ambayo wataweza kutoza wananchi kiasi kidogo cha fedha kutokana na nchi hiyo kuwa na mradi kama huo nchini Dubai.

Maeneo mengine ambayo serikali hiyo imetakiwa kuyaaangalia kuwekeza Balozi Iddi alisema ni ya uvuvi wa kutumia  boti ‘fibre’ pamoja na kuanzisha kiwanda cha kusindika samaki.

Vile vile Balozi Iddi alilitaja eneo jengine ni la kuwapatia wananchi wa Zanzibar nafasi za masomo ambapo kwa kila mwaka iweze kuwasomesha Wazanzibari 10 katika vyuo vikuu vya nchi hiyo kutokana na kuwepo wanafunzi wengi wanaohitaji kujiunga na vyo vikuu.

Upande wa siasa Balozi Iddi alisema ujumbe wao huo uliweza kukutana na Spika wa Bunge wa Nchi hiyo ambapo aliwaalika kuja Zanzibar kuona shughuli za Baraza la Wawakilishi kutokana na nchi hiyo kuwa na mfumo wa Bunge ambapo waliahidi kufanya hivyo.

Aidha balozi huyo alisema uhusiano wa nchi hizo unaongezeka, Serikali ya Zanzibar imetoa mwaliko wa kuitaka nchi hiyo kufungua ubalozi wake hapa Zanzibar jambo ambalo tayari nchi hiyo imelikubali ambapo alieleza karibuni utafunguliwa.

Kuhusu suala la utamaduni wa tamasha la nchi hiyo alisema serikali ya Zanzibar imetowa mwaliko kwa nchi hiyo kuja kuona namna ya utamaduni wa Zanzibar na watavyoweza kushirikiana katika nyanja hiyo kutokana na tamaduni za nchi hiyo kufanana na Zanzibar.

Balozi Seif katika ziara hiyo, amefuatana na viongozi mbali mbali akiwemo Mke wake Mama Pili, Waziri wa Nchi Afisi ya Rais Baraza La Mapinduzi, Dk. Mwinyihaji Makame, Mwakilishi wa Jimbo la Mpendae Mohammed Dimwa, Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo, Bihindi Hamad na baadhi ya watendaji katika Wizara yake.

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s