Wawakilishi watafautiana

Waziri wa Mifugo na Uvuvi wa Zanzibar, Said Ali Mbarouk ambaye ni Mwakilishi wa Jimbo la Gando (CUF) aliposimama kuchangia katika mdahalo wa jumuiya zisizo za kiserikali juu ya umuhimu wa ushiriki wa wananchi na wana azaki katika usimamizi na utekelezaji wa mageuzi ya serikali za mitaa Zanzibar, ambapo alisema sikweli kwamba muundo wa serikali ya umoja wa kitaifa umedhoofisha demokrasia miongoni mwa viongozi wa kuchaguliwa visiwani hapa

MJADALA kuwa mfumo mpya wa serikali ya umoja wa kitaifa Zanzibar umeua au kudhoofisha demokrasia visiwani Zanzibar umeiibuka miongoni mwa wajumbe wa baraza la wawakilishi huku viongozi ndani ya serikali hiyo kutetea kwa nguvu zote mfumo huo.

 Akizungumza katika mdahalo wa kujadili maeguzi katika serikali za mitaa, juzi katika ukumbi wa baraza la wawakilishi mjini hapa, aliyekuwa waziri katika serikali iliyopita ya Zanzibar, Hamza Hassan Juma (CCM) wa Jimbo la Kwamtipura alisema kuwa dhana ya demokrasia Zanzibar imekufa kutokana na kokesekana upinzani ndani ya baraza la wawakilishi.

“Tumepata faida kubwa ya amani na utulivu Zanzibart tu, lakini demokrasia imekufa ndani ya baraza la wawakilishi, huo ndio ukweli. Serikali sasa inakosa kusukumwa na upinzani,” Hamza alisema.

Lakini  Waziri wa Mifugo na Uvuvi wa Zanzibar, Said Ali Mbarouk (CUF) Jimbo la Gando aliposimama kuchangia katika mdahalo huo uliyotayarishwa na Muungano wa asasi Zanzibar (ANGOZA) alisema sikweli kwamba muundo wa serikali ya umoja wa kitaifa umedhoofisha demokrasia miongoni mwa viongozi wa kuchaguliwa visiwani humo.

Alisema badala yake muundo huo umesaidia kujenga na kuimarisha zaidi demokrasia na ndio maana viongozi hao, kupitia CCM na CUF wana mshikamano wa hali ya juu katika kutetea maslahi ya wapiga kura ndani ya Baraza la Wawakilishi.

Mbarouk alisema hivi sasa ndani ya baraza wajumbe (backbenchers) wamekuwa wakitumia vizuri uhuru wao kuibana serikali kwa maslahi ya wananchi na wamekuwa wakileta changamoto kubwa jambo ambalo kwa katika historia ya Zanzibar ni geni.

“Mfano katika kujadili mswada wa utumishi wa umma, serikali ililazimika kurejesha serikalini mswada huo kufanyiwa marekebisho baada ya wajumbe wa baraza kupitia CUF na CCM kuungana kupinga mswada huo,” alisema Mbarouk.

“Mfumo huu utajenga na kuimarisha zaidi demokrasia, tofauti na maoni kwamba utapunguza,” alisema Mbarouk na kutaka ANGOZA iendelee na kazi ya kusimamia asasi za kiraia na kuzipa uwelewa juu ya namna ya kuzibana halmashauri, Baraza la Wawakilishi na Serikali kwa jumla.

Katika mada yake juu ya “ushiriki wa wananchi na asasi za kiraia katika usimamizi wa na utekelezaji wa mpango wa kuleta mageuzi ya serikali za mitaa, Katibu wa ANGOZA, Asha Aboud alisema mpango huo ni sehemu ufanikishaji wa misingi ya dempokrasia na utawala bora.

Asha alisema ushirikishwaji huo una lengo la kutoa fursa kwa wananchi kushiriki kikamilifu katika kubuni mipango ya maendeleo yao, kuitekeleza na hata kutathimini mafanikio ya malengo. “Hali hii huchochea upatikanaji wa maendeleo endelevu kwa njia ya haraka zaidi.”

Mdahalo huo umeambatana na maonyesho ya siku mbili, kuanzia jana, pamoja na maonesho ya kazi za asasi za kiraia zipatazo 50 kwenye viwanja vya Baraza la Wawakilishi, Mbweni Mjini Unguja.

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s