Tunakuungueni mkono wana asasi

Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar, Pandu Ameir Kificho alipokuwa akifungua mdahalo ulioandaliwa na Jumuiya ya Asasi za Kiraia Zanzibar (ANGOZA) jana na kuwashirikisha wajumbe wa Baraza la Wawakilishi katika ukumbi wa baraza hilo huko Mbweni nje kidogo ya Mji wa Zanzibar

SPIKA wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar, Pandu Ameir Kificho amewataka wajumbe wa baraza hilo kuunga mkono juhudi ya asasi za kiraia katika kupigania haki na maendeleo ya wananchi.

Alisema asasi hizo zinatoa mchango mkubwa unaosaidia kuleta mabadiliko katika jamii kwa kuwapa wananchi uwezo wa kutatua matatizo ya maendeleo katika maeneo yao na kuwataka kuendelea na kazi hiyo nzuri walioionesha.

Kificho alikuwa anafungua mdahalo ulioandaliwa na Jumuiya ya Asasi za Kiraia Zanzibar (ANGOZA) jana na kuwashirikisha wajumbe wa Baraza la Wawakilishi katika ukumbi wa baraza hilo huko Mbweni nje kidogo kutoka mjini hapa.

Alisema utendaji wa asasi za kiraia ukiungwa mkono na wajumbe wa Baraza la Wawakilishi na jamii kwa jumla utasaidia kuharakisha upatikani wa maendeleo ya wananchi katika maeneo yao.

Wakati wa mdahalo huo wajumbe wa Baraza la Wawakilishi na wadau wa asasi mbali mbali zinazoshirikishwa na ANGOZA walijadili “umuhimu wa wa ushiriki wa wananchi na asasi za kiraia katika usimamizi wa utekelezaji wa mpango wa mageuzi ya serikali za mitaa, Zanzibar.

Mpango huo wa miaka mitano una lengo la kutoa elimu  juu ya ushiriki wao katika kubuni mipango ya maendeleo inayotekelezwa na serikali za mitaa na kusimamiwa na mabaraza ya madiwani.

“Wananchi wengi hawajui sheria na sera zilizounda serikali za mitaa. Vile vile hawajui mchakato wa utekelezaji wa mchakato wa utekelezaji wa mpango wa kuleta mageuzi katika serikali za mitaa, Zanzibar ,” alisema Katibu wa ANGOZA, Asha Aboud wakati wa mdahalo huo.

 Sambamba na mdahalo huo, ANGOZA pia imeandaa maonyesho ya siku mbili juu ya kazi mbali mbali zinazofanywa na asasi za kiraia Zanzibar .

Maonyesha hayo yanafanyika kwenye viwanja vya Baraza la Wawakilishi, Mbweni na kuwashirikisha wajumbe wa baraza hilo na wadau wengine za kiraia.

Taasisi za kiraia 57, zinashiriki katika maonyesho hayo na 52 zinatoka Zanzibar na tano zinatoka Tanzania bara. Nia ya maonyesho hayo ni kutoa elimu juu ya ushiriki wa wananchi katika usimamizi wa mpango wa mageuzi ya serikali za mitaa Zanzibar ambao unafadhiliwa na taasisi ya Sweden iitwayo The Foundation for Civil Society.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s