Maalim Seif arudi akiwa bukheri-wa-afya

Makamo wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad, akiwa na uso wa furaha baada ya kutua na kupokelewa kwenye uwanja wa Zanzibar akitokea ziara ya muda mrefu ya kiserikali katika nchi za Ulaya na Arabuni na baadaye kupitia India kwa ajili ya matibabu. Maalim Seif amewasili leo Zanzibar na kuzungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa Uwanja wa Ndege.

 

MAKAMU wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Shariff Hamad amesema washirika wa maendeleo wameonesha nia kusaidia ujenzi wa bandari huru katika eneo la Mpigaduri Unguja.

Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kurejea kutoka nchi za nje, Makamu huyo wa Rais alisema “Nikiwa Sharjah tumezungumza kwa kina kuhusu bandari huru, yapo matumaini makubwa ya kufanikiwa katika suala la kujengewa bandari huru”

Alisema bandari huru itasaidia kukuza uchumi wa Zanzibar na pia kupunguza tatizo la ajira kwa vijana huku akisisitiza umakini wa watendaji wa Serikali katika kusimamia miradi ya Serikali.

“Wenzetu wamepiga hatua kubwa sana katika mambo ya bandari huru kwa kweli sisi tuko nyuma sana, lakini tutajitahidi kufika huko bila ya kuwa na umakini hatuwezi kufika” Alisema Makamu wa kwanza wa Rais.

Makamu wa kwanza wa Rais alisisitiza kujengwa kwa miundombinu ya barabara katika maeneo huru kabla ya kuanza kwa mradi huo ili mradi ukija tayari kuwe na miundombinu iliyokamilika.

Alisema kuwepo kwa miundombinu iliyobora kutasaidia kukuza uchumi wa Zanzibar hivyo ni jukumu la watendaji wa Serikali kufanya kazi kwa bidii kufikia maendeleo endelevu.

Maalim Seif alisema kuna kasoro kwa baadhi ya watendaji kutofuatilia miradi ya Serikali licha ya miradi hiyo kukubaliwa na washirika wa maendeleo na amegundua hilo wakati wa mazungumzo na viongozi mbali mbali aliokutana nao katika nchi ambazo ametembelea.

“Kwa upande wa watendaji wetu nao wanaudhaifu katika kufuatilia yale wanayokubaliana na watendaji wenzao” Alisema Makamu wa kwanza wa Rais na kuongeza “Nitakuwa nikiwahoji hatua kwa hatua walizofikia katika kusimamia miradi ya Serikali”

Amesema ameshangazwa baadhi ya nchi zilikuwa zikisubiri ujumbe kutoka Zanzibar kwenda kuendeleza makubaliano ya baadhi ya miradi lakini alichogundua kwamba kuna watendaji walikuwa wakishamaliza mazungumzo hawafuatilii tena jambo ambalo ameahidi kulisimamia yeye na viongozi wenzake.

Amewahakikishia wananchi kwamba atakuwa akiwahoji Mawaziri waliokwenda katika ziara yake kutaka kufahamu maendeleo ya yale waliyokubaliana na wenzao wa nchi walizotembelea na kujua walichokubaliana kama kimetekelezwa au laa.

Katika ziara yake Makamu huyo wa kwanza wa Rais alisema amefanya mazungumzo rasmi na viongozi wa nchi za Uholanzi, Falme za Kiarabu ambapo wengi wameonesha nia ya kusaidia miradi mbalimbali ya maendeleo Zanzibar.

Alisema amezungumza na Naibu Waziri Mkuu wa Oman ambaye amemuhakikishia dhamiya ya nchi hiyo kushirikiana na Zanzibar kwa kuwa wazanzibari ni wenzao hivyo hawataona tabu kuwasaidia huku akiahidiwa mashirikiano ya kusaidiwa ofisi ya wakfu kwa kubadilishana uzoefu wa shughuli hizo.

Baadhi ya miradi ambayo wameuzungumzia ni pamoja na uanzishwaji wa viwanda vya samaki, kubadilishana wanafunzi kati ya chuo kikuu cha taifa cha Zanzibar (SUZA) na chuo kikuu cha Sharjah, Zanzibar kuwasomesha wanafunzi wa Kiswahili ambapo kutakuwa na mikataba maalumu wa mafunzo hayo.

Ziara ya Maalim Seif pia imefungua mahusiano mapya kati ya Zanzibar na Uholanzi baada ya kutetereka kidogo mahusiano hayo ingawa hakutaka kuwa muwazi katika suala hilo kwa kusema kwamba ni masuala ya ndani lakini alisema ameweza kurejesha mahusiano baada ya mazungumzo yake na viongozi wa nchi hiyo.

Eneo lake la mazingira na kupambana na madawa ya kulevya pia limezungumziwa katika safari yake pamoja na suala zima sugu la upatikanaji wa maji safi na salama ambapo kwa kiasi kikubwa amesema baadhi ya nchi zimekubali na hivi sasa kunafanywa tathimini ya upatikanaji wa maji hapa Zanzibar ili wajue namna gani watakavyoweza kusaidia suala hilo.

Hata hivyo Makamu huyo wa kwanza amesema kitu muhimu kwa sasa ni kuwa na umakini ili miradi na makubaliano yote yanayofungwa na nchi wafadhil iwe inafanyiwa kazi na akasisitiza uwajibikaji wa watendaji katika kuhakikisha miradi yote inafanyika kwa mujibu wa makubaliano yaliofikiwa.

“Sasa hakuna mchezo tena, sasa ni utekelezaji ndio unaotakiwa tumekwenda kutafuta msada na tunatakiwa kuifanyia kazi ili kila tulichokubaliana kiwe kinaekelezwa” alisema Maalim Seif ambaye alikuja kupokewa na mkuu wa mkoa wa mjini magharibi Abdallah Mwinyi Khamis na mawaziri mbali mbali.

Malim Seif alikuwa nje ya nchi kwa muda wa wiki saba ambapo wiki nne alikuwa katika ziara za kiserikali na kutembelea Uholanzi alipokwenda katika mkutano, Sharjah, Dubai na Oman na wiki tatu za mwisho alikwenda kukagua afya yake ambapo alipatikana na tatizo la kiafya na kulazimika kufanyiwa upasuwaji wa goti nchini India.

One response to “Maalim Seif arudi akiwa bukheri-wa-afya

  1. bi salma asante na lakini unakumba ukiandiklie mahojiano baina ya maalim seif na waandishi wa habari

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s