Mamlaka ya Sheha yapitiwe upya

Wazanzibari wengi hupenda ikifika asubuhi kwenda eneo la Darajani maarufu masomo book shop kutizama vichwa vya magazeti yalivyoandika lakini idadi kubwa wamekuwa ni watizamaji tu wa vichwa vya habari wanunuzi wa magazeti ni wachache kutokana na sababu mbali mbali ikiwemo ukosefu wa fedha khasa kwa kuzingatia kuongezwa kwa na magazeti ambapo kwa sasa bei za magazeti ni shilingi 500

IMEELEZWA kwamba licha ya kuwepo Serikali ya umoja wa kitaifa Zanzibar sheria inayoanzisha mamlaka ya sheha bado haijafanyiwa marekebisho kwa kadri ya nyenendo za siasa za Zanzibar zinavyokwenda.

Hayo aliyasema Mhadhiri wa chuo kikuu cha Dr es Salaam Professa Lupa Ramadhani wakati akitoa mada ya nafasi na wajibu wa sheha katika serikali ya kitaifa iliyofanyika ukumbi wa hoteli ya Bwawani Mjini Zanzibar na kusema kwamba ni lazima ibadilishwe ili iendane sambamba na mabadiliko mapya ya serikali ya umoja wa kitaifa..

Alisema mara nyingi masheha wamekuwa wakilalamikiwa kwa upendeleo hasa katika siku za chaguzi na hata katika shughuli za kila siku katika maofisi yao kwamba wamekuwa wakipokea amri za chama tawala na kukataa kuwahudumiwa wanachama wa vyama vyengine jambo ambalo ni kinyume na sheria kwa kuwa kwa mujibu wa sheria za sheha yeye ni mtendaji wa serikali na sio mtendaji wa chama..

Akifafanua zaidi amesema kwa ujumla kazi za utendaji wa sheha unatakiwa uwiyane na hali halisi ya siasa za maridhiano kutokana na kuwa serikali iliyokuwepo inaundwa na chama zaidi ya kimoja hivi sasa baada ya kuja mfumo huo uliotanguliwa na kura ya maoni.

Professa huyo alisema ni vyema elimu itolewa kwa masheha wote kuhusu serikali ya umoja wa kitaifa kupitia wajumbe wale wajumbe sita wa baraza la wawakilishi ambao wametunukiwa tunzo ya serikali ya marekani kwa kufanya kazi nzuri ya kuhakikisha maridhiano yanasimama Zanzibar..

Kwa upande wake muhadhir kutoka chuo kikuu cha Zanzibar (SUZA) Ali Haji Vuai alisema si vibaya kama serikali itafanya marekebisho ya mamlaka ya serikali za mikoa ili kupitia upya vigezo vya uteuzi wa nafasi ya masheha vilingane na hali ya sasa ya serikali iliyopo ambayo ina sura mpya katika muundo wake.

“Ni vyema serikali kupitia upya sheria ambazo zinamuweka sheha kwenye migogoro ya kimaslahi au katika kutumikia kisiasa kama vile sheria za uchaguzi na kupima faida na hasara za kuwepo kwa sheha kwenye mchakato wa uchaguzi”alisema Vuai.

Sambamba na hilo amevitaka vyama vya siasa kuacha kumtumia sheha kwa maslahi yao binafsi ya kisiasa na wamuachie aendelee kuwa mtu wa kuitumikia serikali kwenye jamii akiwa kama nembo ya umoja na maelewano, na masheha kwa upande wao wasikubali kutekeleza maagizo yaliyo nje ya sheria zao za kazi

Vuai alisema ni muhimu kwa masheha wenyewe kujielimisha na taasisi mbali mbali kutoa mafunzo ili waweze kutimiza majukumu na matarajio ya kuwepo kwao katika jamii ili waweze kujenga imani ya jamii na kuleta maendeleo.

Aidha aliitaka jamii nayo kutoa mashirikiano kwa masheha na kusahau yaliyopita na kuangalia mbele si vizuri kuendeleza visasi ambavyo vinagharimu juhudi za kuleta maendeleo hapa nchini. 

Wakichangia washiriki katika mjadala huwo wamesema wananchi wana wajibu wa kubadilika na kukubali masheha ni watawala na si vyema kumbagua kwani kufanya hivyo kutaleta mashirikiano madogo baina ya masheha na wananchi.

Aidha wamesema baadhi ya wananchi wanatumia nafasi ya utashi wa siasa kwa kutotoa mashirikiano baina yao na masheha kwa madai ya kutowatambua na kupelekea kukosa haki nyingi zinazotokana na sheha. Wamesema nafasi ya masheha ni kulinda kutii amri ya serikali kiutendaji na kufanya kazi kwa niaba ya serikali kwa lengo la kuhudumia wananchi.

Kutokana na ugumu wa kazi za masheha kuna vikwazo ambavyo vinasababishwa na misingi ya vyama mfumo wa vyama vingi si mbaya lakini mapokezi yamepokewa vibaya huku nafasi ya sheha kiutendaji wake huonekana mbaya kutokana na kukosa mashirikiano na ngazi za chini kwa dhana ya siasa.

Pia kuna upugufu wa sheria ambazo masheha huonekana ni kikwazo ambayo utekelezaji wake unamfanya sheha aonekane utendaji wake ni mbaya.“Tunaomba wasomi wa chuo kikuu mteremke kwa masheha kutafuta ukweli uliopo sasa tushirikiane kwani sote ni watumishi wa serikali”.alisema mchangiaji mmoja katika semina hiyo.

Warsha hiyo ya siku mbili kuhusu nafasi na wajibu wa masheha katika serikali ya umoja wa kitaifa imetayarishwa na chuo kikuu cha Dar- es- Salam mpango wa utafiti na elimu ya Demokrasia Tanzania (REDET).

Advertisements

2 responses to “Mamlaka ya Sheha yapitiwe upya

  1. Ninapopita kwenye sehemu za uzwaji wa Magazeti nikaona watu wanayakodolea macho hisia zangu nikuwa uwezo mdogo lakini hamu na ghamu ya kusoma magazeti ipo. Ninapopita kwenye Kioski au Mkahawa au Nyumba mtu akaweka TV yake kisha kundi la watu wapo wanaangalia, hiyo kwangu mie ni UMASIKINI, hutonpeleka kwenye maskani nikajiweka niangalie TV wakati nina uwezo wakuiyona kwangu.
    Hivi ni viashiria vya umasikini vinahitajia kufanyiwa kazi.

    Ben Rijal

  2. ndio moja ya faida za muungano ati leo znz mtu hawezi kununuwa gazeti au hana tv aende maskani akangaliye tv wakati wa MZEE KARUME aliwapa watu wote tv kisha walipe kidogo kidogo ndio kuwapenda wananchi wako sio kuwawakeya tv moja kisha wote wako hapo wanaikodoleya mijicho 2011 bado tunaisha kama tuko ktk mwaka 1590 kisha tumendeleya na muungano wetu mawe tutarudi nyuma kila kukicha na muungano feki

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s