Sheria inaniruhusu kuwa jaji-Hamid

Jaji Mkuu Hamid Mahmoud amejibu barua aliyoandikiwa na Chama Cha Wanasheria Zanzibar (ZLS) wakisema wadhifa alionayo ni batili kisheria

JAJI Mkuu Zanzibar, Hamid Mahmoud amesema katiba ya Zanzibar inamruhusu kuendelea na wadhifa huo, baada ya kuongezewa mkataba na Rais, licha ya kuwa alikwisha staafu kwa hiari na kulipwa mafao yake.   

Jaji Mkuu amesema hayo katika barua yake kwenda kwa Katibu Mkuu wa Baraza la Mapinduzi kujibu hoja za Chama Cha Wanasheria Zanzibar(ZLS) waliotoa indhari kwa serikali juu ya azma yao ya kufungua kesi kupinga uhalali wa kuendelea kuwa katika nafasi hiyo.

Jaji Mahmoud katika barua barua hiyo ambayo gazeti hili imeona nakala yake alisema baada ya kustaafu kuna kazi ambazo alikuwa bado hajazikamilisha na kwa kutumia kifungu cha 95(3) cha Katiba ya Zanzibar aliongezewa muda ili kukamilisha kazi hizo.

Jaji Mahmoud katiba baru yake hiyo ya Machi 17, mwaka huu yenye kurasa saba alikikariri kifungu hicho cha Katiba kuwa “Licha ya kuwa Jaji amefikia umri ulioainishwa katika kifungu cha 95 (1), Jaji wa Mahakama Kuu ataendelea katika wadhifa wake huo mpaka pale atakapomaliza shughuli zote zilizomfikia kabla ya kutimiza umri huo.

Kwa msingi huo jaji Mahmoud amesema kuendelea kwake na kazi katika wadhifa huo ni halali kisheria na hakujakiuka kifungu chochote cha katiba na hapakuwa na haja ya kuteuliwa Jaji wa Mahakama Kuu na baadaye kupendekezwa tena kuwa Jaji Mkuu kama inavyodaiwa na chama cha wanasheria.

Alisema katika mkataba wake huo mpya inaelezwa wazi utaratibu utakaotumika kuhusu malipo baada ya kuwa amestaafu na analipwa pencheni katika muda huo wa miaka miwili hadi April 30 mwaka huu.

“Mkataba huu umeeleza kuwa nilipwe kile tu ambacho silipwi katika malipo yangu ya pencheni, mengine yaliyomo ni kama yalivyo katika utumishi wangu katika nafasi hiyo, kama vile haki ya kupata likizo na malipo ya muda wa ziada nitakaokuwa nimefanya kazi baada ya kustaafu”, alisema katiba barua yake.

Aidha, alisema kwamba hakuna msingi wowote kwa chama cha wanasheria Zanzibar kuitaka mahakama imtake Rais wa Zanzibar aunde tume ya kuchunguza uhalali wa kuendelea kushika wadhifa wa Jaji Mkuu.

Alisema mahakama haina uwezo wa kisheria kumpa Rais amri yoyote ile hasa kwa kuzingatia uamuzi wa mahakamani hutolewa kwa mtu ambaye anafikishwa mahakamani na kupewa nafasi ya kujitetea.

Jaji mkuu alieleza kwa vile hakuna sheria ya kumfikisha mahakamani Rais awapo madarakani na kwa maana hiyo hakuna uwezekano kwa mahakama kumuamuri Rais aunde tume.

Akizungumzia hoja za Jaji mkuu, Rais wa chama cha wanasheria Zanzibar, Yahya Hamad alisema hoja za chama hicho ni kwamba utaratibu mzima wa kumuongezea mkataba ulifanyika kinyume na ibara ya 94(1) ya Katiba ya Zanzibar.

Alisema baada ya Jaji Mkuu kustaafu kwa hiari hakuna kikao cha Tume ya Utumishi wa Mahakama ambayo kiliwahi kujadili mkataba wake wa kazi na kuupitisha, wakati tume ya utumishi wa mahakama kwa mujibu wa katiba ndiyo yenye jukumu la kujadili na kupitisha mkataba huo.

Aidha, Yahya alisema kwamba baada ya kustaafu kwake kwa hiari alitakiwa ateuliwe tena kuwa jaji wa mahakama kuu na ndipo aongezewe tena mkataba wa kuwa Jaji Mkuu, jambo ambalo halikufanyika na ni kinyume na katiba ya Zanzibar.

Rais huyo alisema kwa kuwa uteuzi wake umekiuka katiba na ndio maana wanaiomba mahakama itangaze kuwa kuwepo kwake kwenye wadhifa huo ni batili kwa mujibu wa katiba ya Zanzibar na serikali ikubaliane na hoja zao.

Advertisements

2 responses to “Sheria inaniruhusu kuwa jaji-Hamid

 1. Nahisi hawa watu wanaokinzana wote ni nwanasheria mahiri kwa hivyo kwetu sisi tusiokuwa katika kundi hilo wanatuchanganya tu. Nashauri hawa watu wakae pamoja na kulitatuwa hili kisheria na waache malumbano yasiyo na tija .

  Ahsante.

 2. Tanbih kwa Wanasheria. Liliopo ni sio Jaji Mahmoud kurejeshwa kazi, bali ni kwanini watu wanafikia umri wa kustaafu Wanaume miaka 60 na wanawake miaka 55 kisha ukajasikia mtu anaongezewa mkataba hli ndio la kulizingatia na kulikalia kidete.

  Nilionalo mie Jaji Mahmoud kisha pata nafasi na hivyo ndivyo tulivyo, bali Wanasheria mloukuwa wakakamavu na kutufumbua macho kina sisi Pangu Pakavu kwa mengi ambayo munatuzindua, nikionacho muishauri Serikali kuwa akifika mtu kastaafu basi awe amestaafu, inagawa na mie binafsi siko mbali na wimbi hilo.

  Aliostaafu kama ujuzi wake utakuwa unahitajiwa kweli-kweli basi aitwe kila panapohitajika, wala sio achukue nafasi ambayo vijana wapo na wanabakia bila ajira.

  Museveni wa Uganda anataka kurekebisha katiba uwe umri wa kusataafu miaka 55 ili kutoa fursa kwa damu changa nao kupata fursa ya kuajiriwa.

  Sahib mmoja kule Pemba aliwahi kuniahadithia alipokuwa ansoma Secondary school, alikuwa mzee mmoja anafanya kazi katika Ofisi fulani ya Ardhi, akamaliza masomo ya High school, akajiunga na hiyo Idara akawa pamoja na huyo mzee, kisha akenda kufanya Advance Diploma, akenda kufanya Master Degree, chakuchekesha kijana huyo akawa yeye ana umri mkubwa koliko yule mzee ambaye yeye yupo Secondary School mzee mkukuu kazini.

  Ushauri wangu katika hili ni kuangaliwa watu umri wao. Zanzibar kumekuwa na mtindo wa watu kujirejesha umri nyuma, na hayo yanakuja kuwa watu wanalipwa kijimshahara cha Chuuuu, ambacho hakimfikishi mtu mwahali, kwamaana hiyo na Pencheni siochochote wala lolote lile. Anapostaafu mtu huyona Mauti yale pale. Anachukua kila mbinu abakie kazini, baada ya wenzetu pale anapoambiwa anastaafu anasikia raha kabisa.

  Wanasheria Jaji sisemi muachieni lakini la Jaji ni duchu, kubwa ni hili ambalo wastaafu kupewa Mikataba.

  Ndivyo aonavyo
  Ben Rijal

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s