Second hand zahofiwa kuharibu mazingira

Televisheni na radio ambazo zimekuwa zikiletwa hapa Zanzibar na kuuzwa ambazo wananchi wengi wenye kipato cha chini ndio imekuwa tegemeo lako hivi vifaa vya second hand kwa kiasi kikubwa vifaa hivi vinaonekana kuathiri mazingira hapa nchini kutokana na kukosekana mbinu za kuviteketeza bila ya kuathiri mazingira

SERIKALI ya Mapinduzi Zanzibar imesema  inakabiliwa na ongezeko kubwa la vifaa vya chakavu vya electroniki ambavyo kwa kiasi kikubwa vinaweza vikaleta athari kubwa za kimazingira hapo baadae iwapo vitaachwa kusambaa hapa nchini.

Kauli hiyo imetolewa na Mrajis wa Tume ya Utangazaji Zanzibar, Abdallah Hassan Mitawi wakati akizungumza na ujumbe kutoka afisi ya makamo wa kwanza wa rais wa Zanziba ulipofika ofisini kwake kuzungumza nao.

Mitawi alisema zaidi ya redio laki tisa na themanini (980,000) pamoja na Seti za televisheni laki tatu (300,000) za aina ya analogi zimo hapa Zanzibar ambazo baada ya muda mfupi hazitatumika tena kutokana na teknojia hiyo kuachwa kutumiwa tena duniani.

Alisema tatizo liliopo hapa Zanzibar hakuna sehemu ya kutupa idadi ya vifaa hivo chakavu na bado nyengine kwa wingi zinaendelea kuletwa baada ya kukithiri biashara ya vifaa vilivyokwisha tumika kuingizwa nchini (Second hand) ambavyo kuna matarajio ya kuharibika zaidi hali ya mazingira iwapo vitaachwa kuingia nchini.

Alisema baadhi ya nchi duniani zimeacha kutumia vifaa hivyo lakini pia nchi hizo zinazo uwezo wa kukabiliana na vifaa hivyo visivyotumika kutokana na kuwa na mashine za kuvifaribu na kuvibadilisha na kuoathiri mazingira na nchi hizo jambo mbalo Zanzibar bado haina utaalamu huo wala zana hizo za kuumia ili wasiharibu mazingira.

Kutokana na ongezeko la vifaa hivyo chakavu kuna tatizo jipya la ongezeko la madawa ya sumu kutokana kutupwa ovyo taka taka hizo za vitu vyenye kemikali imeelezwa.  

.

Mrajis huyo alisema tume yake imejipanga katika kutekeleza hayo kwa kutoa mafunzo kwa vyombo vya habari na lazima viwe tayari katika kuyataekeleza hayo kwa kufuata sera na kanuni zilizopo nchini.

Nae Katibu Mtendaji wa Tume ya Utangazaji, Chande Omar alisema huu ni wakati muafaka kwa vyombo vya habari kuelimisha jamii juu ya umuhimu wa kuweka usafi wa mazingira katika maeneo yote yanayotuzunguka na kutolewa elimu ya madhara ya kemikali zitokanazo na vifaa hivyo vinavyoingizwa nchini.

“Tunatafuta ni namna gani tutaweza kulinda mazingira juu ya vifaa vinavyoingia nchini ambavyo havitumiki lakini vimezagaa kama taka taka ili kuihami nchi yetu na matatizo na janga la kimazingira”alisema Chande.

Alisema kwa sasa nchi yetu haina teknologia ya kuhifadhi sumu za screen ambazo ni uchafu unaotokana na taka taka zilizotupwa na huenda madhara yake yakajitokeza baadae bila ya wananchi kuelewa.

Kwa upande wake Waziri kutoka ofisi ya Makamo wa kwanza wa Rais, Fatma Abdul-habib Ferej alisema majukumu yote ambayo ofisi yake imepangiwa yanagusa jamii moja kwa moja kutokana na umuhimu wake wa maisha ya kila siku yanayoigusa jamii.

Ili kutekeleza majukumu hayo mashirikiano kati ya ofisi yake na taasisi zote za  habari ikiwemo vyombo vya habari vya serikali na binafsi yanahitajika ili kutoa elimu kwa umma juu ya kuhifadhi na kujihami na matatizo yanayoweza kujitokeza kutokana na uchafuzi huo wa mazingira.

Ferej alisema ili kuyafanikisha hayo ni lazima kujenga mashirikiano hayo hususan kwa vyombo vya habari kwa kuwa vina umuhimu pekee wa kuielimisha jamii na vina nafasi kubwa katika kuilimisha umma.

Alisema majukumu ya ofisi yake ni pamoja na mambukizi ya ukimwi, madawa ya kulevya, walemavu na mazingira ambapo mambo yote hayo yanawagusa jamii moja kwa moja ikiwa hayakutolewa elimu yatakuwa na ugumu wa utekelezaji wake.

Matumizi ya teknologia mpya ya vyombo vya habari Analog kwa kiasi kikubwa yameanza kuachwa ulimwenguni kote baada ya kuja mfumo mpya wa teknologia ya mawasiliano ya Digital, lakini bado vyombo vya habari vya serikali vinaaendelea kutumia mfumo huo mkongwe wa analogi hadi sasa.

Matumizi ya vifaa vya analogi vitafikia ukomo wake hapo ifikapo mwaka 2020 duniani kote ambapo kwa kiasi kikubwa nchi nyingi hivi sasa zinaendeleo kutumia mfumo mpya wa digital katika vyombo vyake vya habari ikiwemo redio na televisheni lakini hapa Zanzibar bado wanaendelea kutumia analogi.

Advertisements

One response to “Second hand zahofiwa kuharibu mazingira

  1. Zanzibar na nchi nyengine za Ulimwengu wa 3 lazima zitafakari dhana nzima ya kupatia watu wake ASJIRA. Kwakuwa tu watu watapata kazi au pesa maisha ya Uma hauna thamani. Nakumbuka Ivory Coast walipokea taka za sumu kwa uroho wa pesa na arwah za watu zikapotea.

    Leo Zanzibar limekuwa jaa kuu la vyombo mbalimbali chakavu, iwe magari, baskeli, TV na Radio. Pemba nako kwa mukhtadha wa ajira watu wanapasua Miamba kupatikana Matufali ya kujengea. Linalohitajika ndani ya nchi yetu tuwe wakweli, tujuwe nchi yetu hii tumewanadalia nini kizazi kijacho, mazingira yetu tunayadhibiti vipi.

    Kabla ya hata kuwekwa Sheria Serikali inaweza kupiga marufuku uingizaji wa Mitumba yote ya Elektroniki wala kutomsikiliza yoyote yule, na Serikali hilo wanaliweza. Helmet aina mpya watu wameshatakiwa kununua na kuzivaa hilo ni toleo la Serikali na utakuta sheria hiyo itatekelezwa. Verejee mazito kama haya ya Mitumba ya Elektroniki yawe mazito kuchukuliwa hatua?

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s