Majambazi kumi wakamatwa Zanzibar

Bandari ya Malindi Zanzibar imekuwa ikitumika sana kwa wasafiri kutoka sehemu mbali mbali na kuja kutembea na kwa shughuli za kibiashara lakini pia imekuwa ndio njia kuu wanaotumia wahalifu wenye kuja kufanya vitendo viovu hapa Zanzibar na hayo yote yanatokana na kuondoshwa kwa pasi ya kusafiria imekuwa Zanzibar watu wanaingia na kutoka ovyo bila ya kuwepo vidhibiti vyovyote

JESHI la Polisi Mkoa wa Kaskazini Unguja linawashikilia watu 10, wanaosadikiwa kuwa ni majambazi ambao walikuwa kwenye maandalizi ya kutaka kupora katika hoteli ya kitalii ya My Blue, iliyoko Nungwi Mkoa wa Kaskazini Unguja.

Kwa mujibu wa Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kaskazini, Henry Mwibambe, alisema tukio hilo limetokea majira ya saa tisa usiku wa kuamkia jana, huko Nungwi ambapo hivi sasa matukio kama hayo yaliaza kupungua lakini sasa ameanza kujitokeza kwa kasi hasa huko Tanzania Bara.

Kamanda huyo aliwataja watuhumiwa wa ujambazi hao ni Andrew Henry Yussuf (24) mkazi wa Kigamboni Dar es Salaam, Abdullah Khatib Makota (33), mkazi wa Kiembesamaki, Khamis Msoma Masanja (31), mkazi wa Welezo, Faki Makame Faki (40) mkazi wa Kariakoo, Dar es Salaam.

Wengine ni Salum Seif Roto (30), mkazi wa Manzese Dar es Salaam, Lelo Michael Ringo (31),mkazi wa Tabata, Dar es Saalam, Said Juma Rashid (35) mkazi wa Magomeni Unguja, Msafiri Ali Mengi (25), mkazi wa Jang’ombe, Jeremia Joseph Michael (31), mkazi wa Dodoma na Khamis Kombo Juma (34) mkazi wa Tomondo Unguja.

Aidha Kaimu huyo alisema mmoja kati ya watuhumiwa hao alikamatwa akiwa amevaa sare za kamili za jeshi la polisi ambaye alikuwa katika kundi hilo la watuhumiwa hao.

Alisema mara baada ya majambazi hao kuingia katika hoteli hiyo walijaribu kuwapambana na walinzi wa hoteli hiyo kabla ya kikosi maalum cha kupambana na uhalifu kufika katika eneo hilo na kuanza kuchukua hatua za kupambana nao.

Kaimu kamanda huyo alisema hata hivyo katika kupambana na walinzi wa hoteli hiyo hakuna mtu aliyejeruhiwa hata mmoja, isipokuwa majambazi hao walitumia mapanga na kuwapiga mabapa walinzi hao kwa lengo la kuwatisha na kutaka watulie ili watimize azma yao hiyo ya uporaji.

Kaimu huyo ambaye ni Mkuu wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai ya Mkoa huo, alisema Polisi walifanikiwa kuwakamata majambazi hao baada ya kupokea habari za uvamizi hu kutoka kwa wasamaria wema na dhana ya polisi jamii kufanya kazi.

Alisema baada ya polisi kuingia kwenye eneo la hoteli hiyo majambazi hao walijaribu kutoroka kwa kutumia gari yenye namba za uzajili Z 490 AV, Super Custom akuondesha kwa kasi.

Henry, alisema kukimbia kwao kwa kasi majambazi hao haikufanikiwa kwani waliwekewa kizuizi cha barabarani katika kituo cha polisi Nungwi ambapo kikosi cha kutuliza ghasia cha Mkoa huo kwa kushirikiana na polisi wa kituo hicho walifanikiwa kuwadhibiti na kuwaweka chini ya ulinzi mkali majambazi hao.

Alisema watuhumiwa hao wa ujambazi wamekamatwa wakiwa na silaha za jadi kama vile mpanga, ndondo, pamoja na koleo ya kuvunjia milango kwa lengo la kutaka kufanyia uhalifu wao.

Henry alisema watuhumiwa hao inasadikiwa kuwa ndio walioshiriki kuvamia hoteli ya kitalii ya Waridi iliyoko Pwani Mchangani Machi 17 mwaka huu majira ya usiku wa manane na kufanikiwa kuiba vitu kadhaa baada ya kuwafunga kamba walinzi wa hoteli hiyo na kutimiza azma yao.

Alisema kwamba watuhumiwa hao watafikishwa mahakamani mara tu baada ya upelelezi kukamilika, huku Kaimu huyo akiwataka wananchi kushirikiana na Jeshi lake ili liweze kuvunja mtandao wa majambazi ambao umeanza kurudi upya hapa Zanzibar.

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s