Kampeni Zafanywa Vijiweni Pemba

MGOMBEA urais wa Zanzibar kwa tiketi ya chama cha wakulima (AFP) Said Soud Said ameanza utaratibu mpya wa kufanya kampeni kila penye mikusanyiko hadi kwa wakulima wakiwa mashambani mwao.

Hatua hiyo imekuja kufuatia mgombea huyo kubakiza mikutano minne tu ya hadhara iliyoidhinishwa na Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) kabla kufanyika uchaguzi mkuu disemba 31 mwaka huu.

Maeneo ambayo mgombea huyo ameyalenga kwa utaratibu huo wa aina yake pamoja na kwenye masoko, vijiwe vya kahawa, magenge ya vijana na kwa akina mamalishe wa maeneo mbali mbali.

Akiongea na waandishi wa habari mgombea huyo anayetumia pikipiki mbili moja yake na nyengine ya mlinzi wake anasema analenga zaidi mashambani kutokana na wakulima kuwa na idadi kubwa ya kura.

“Kwangu wakulima ni kundi muhimu asilimia 70 ya wazanzibari ni wakulima na ambao wanatoa mchango mkubwa wa pato ya taifa” alisema Soud.

Mgombea huyo amesema uaratibu huo mpya utamsaidia sana kunadi sera za chama cake na kujitangaza kwa wapiga kura na kuongeza kwamba ni njia moja wapo ya kuwajali.

Kwa mujibu wa ratiba malaumu ya ZEC chama hicho kimeakiza mikutano yake katika kijiji cha Pujini octoba 25, Micheweni octoba 27, Kiuyu Minungwini octoba 29 na Wawi ocoba 30 mwa huu.

Hata hivyo kifungu cha 56 (2) cha sheria ya uchaguzi namba 11 ya mwaka 1984 ni wakala au chama cha siasa cha mgombea ndio wanawajibika kuwasilisha ZEC mapendekezo yao ya ratiba ya kufanyika mikutano ya kampeni inayoonesha nyakati na mahala itakapofanyika mikutano hiyo.

Katika hatua nyengine wakati siku zikiwa zinakaribia za kufanyika uchaguzi mkuu baadhi ya wagombea ubunge, uwakilishi na udiwani wa vyama vingi hapa kisiwani Pemba hadi sasa wameshindwa kufanya hata mkutano mmoja wa kampeni kutokana na ukosefu wa fedha.

Wakizungumzia hali hiyo hapo hapo jana Masoud Ally Naasor mgombea wa ubunge Jimbo la Ziwani kwa tiketi ya NLD na Abbass Mohammed Jimbo la Chake Chake wa chama cha UDP wamedai hali hiyo ni kudumaza demokasia.

Wamesema kwamba pamoja na gharama walizopata za kuchukua na kugharamia fomu za maombi vyama vyao kukosa ruzuku kupelekea kutowafikia wapiga kura na hivyo kuwanyima fursa.

“Hatuwezi kusema demokrasia imekuwa Tanzania mfano hapa Pemba CCM na CUF peke yao ndio wagombea wao wenye uwezo wa kufanya kampeni kama vile wana haki miliki ya siasa kwa Pemba” alisema kwa hasira mgombea huyo.

Hivi karibuni wagombea urais wa Zanzibar kupitia vyama vya TADEA, NCCR Mageuzi, AFP, Jahazi Asilia vilipaza sauti zao kuzilaumu tume za uchaguzi za ZEC na NEC kwa kushindwa kuwapa ruzuku na hivyo kutoweza kufanya mikutano kama ratiba zao zilivyoonesha.

Leave a comment